Tuesday 21 September 2010

MAHESABU MAKALI KABLA HUJAJIINGIZA KWENYE CRIME

vukishapiga hesabu hizi na kisha kila dakika ya mwisho jibu unapata -1000 mara -100000 mara -10000000,tena -100000000,yaani wewe kila siku ni minus,minus tuuu hakuna siku unapata plus.wakati wenzio watoto wa vigogo na mafisidi hata huelewi unashangaa wana-change migari tu ya mamilioni na mabilioni na mibangaloo ya ghorofa  vyumba 16 ndani na mabafu matano,tv plasma mabafuni vyooni mpaka kwenye corridor halafu unakuta jamaa mwenyewe bachela anaishi peke yake,wakati wewe kila siku unawaza itaisha vp maana ni mitihani tu,menyu dagaa,tembele,ndondo,mchicha,dengu siku umepata sana umejidai na kambale ama makwasu-kwasu au ndaza(nyama ya juzi au jana na yenye mifupa kibao) we mtu.sijui lini maskini huyu atajikomboa na maisha ya dizaini hii.ndio maana ikifika kipindi cha uchaguzi kile chama chetu kileeee CCC wanaangusha PILAU la kufa mtu na SODA wanajua kwa ukame wa wananchi walio wengi,utu unawatoka hawafikirii hata wanafanya nini zaidi ya kwenda kuuza utu wao na kukipigia kura hicho chama na wagombea wake kwa asilimia 99.9. kama wale wananchi wa monduli.baada ya hapo ni kusikilizia maumivu na kulipia hilo pilao kwa miaka 10 ambayo huyo mgombea kashinda.mwisho ni huyu mnyonge kujiingiza kwenye ukabaji,ujambazi,utapeli kuuza unga na kila aina ya uharamia unaoujua weye,sijui lini tutajikomboa

No comments:

Post a Comment