Friday 16 March 2012

MADARAKA NYERERE AMTOA NISHAI MKAPA NA KUKIRI VICENT NI MDOGO WAO

ASEMA VINCENT NI MDOGO WAO, ATAKA TUHUMA ZINGINE AJIBU MWENYEWE
Waandishi wetu, Dar, Arumeru
MADARAKA Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ameibuka na kuthibitisha kuwa Mbunge wa sasa wa Musoma mjini (Chadema), Vincent Nyerere ni mdogo wao na mwanafamilia hiyo, kwani ni mtoto wa baba yao mdogo, Josephat Kiboko Nyerere.
Kauli ya Madaraka imekuja siku chache baada ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, kudai kwamba hamtambui mbunge huyo kuwa ni miongoni mwa familia ya Mwalimu Nyerere kwani katika kipindi chote alichofanya kazi na Mwalimu, hakusikia jina hilo.
 
Jumatatu ya wiki, akizindua kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, Mkapa aliuambia umati uliohudhuria kwamba hakuwahi kusikia kama kulikuwa na mtoto wa familia hiyo aliyekuwa akiitwa Vincent Nyerere.
 
Kauli hiyo ilipingwa vikali juzi na Vincent akisema si jambo la ajabu Mkapa kutomfahamu yeye kwasababu Mkapa si sehemu ya ukoo wao huku akimrushia kombora kwamba akiwa madarakani alishinikiza Mwalimu Nyerere kupelekwa Hospitali ya St Thomas, Uingereza, kinyume na matakwa ya familia yao na wakati huo huo, daktari wake Profesa David Mwakyusa alijua maradhi ya mwasisi huyo wa taifa.
 
Vincent alikwenda mbali zaidi na kumshambulia Mkapa kwa kuongoza ubinafsishaji holela enzi za utawala wake huku akimtuhumu kuuza viwanda na rasilimali za nchi kwa kisingizio cha ubinafasishaji.
Jana gazeti hili liliwasiliana na Madaraka kutaka kupata ukweli wa kauli hiyo ya Mkapa. Katika jibu lake fupi, Madaraka alithibitisha kuwa.... Soma zaidi:

No comments:

Post a Comment