Friday 9 March 2012

Wauguzi waliogoma wafutwa kazi Kenya


Wauguzi Kenya wakisaidia wagonjwa, 25,000 waliogoma wafukuzwa kazi
Serikali yaKenya imewafukuza kazi wauguzi 25000 waliogoma kwa kushindwa kurudi kazini.
Msemaji wa serikali Alfred Mutua ametoa wito kwa ‘ watu wenye taaluma ya afya wote’ ambao hawana ajira au waliostaafu kufika hosiptali za umma kwa ajili ya kuajiriwa siku ya Ijumaa.

Wafanyakazi wa umma ambo wengi ni manesi waligoma tangu wiki iliyopita wakitaka kupandishiwa mishahara, marupupurupu na kuboreshewa mazingira ya kazi.
Vyama vya wafanyakazi wamepuuzia hatua hiyo wakisema ni mbinu ya kuwataka wajadiliane.
"Huu ni mchezo wa paka na panya, huwezi kuwafuta kazi wafanyakazi wote. Ni mbinuyaotu ya kutufanya haraka turudi kazini lakini mgomo wetu unaendelea mpaka madai yetu," Shirika la habari la Reuters limemnukuu Alex Orina, msemaji wa Taasisi ya wanataaluma wa afya akisema.
Alisema kwa wastani mfanyakazi wa sekta ya afya anapata kiasi cha shilingi 25,000 zaKenya($300, £190) kwa mwezi kwenye mshahara wake na posho.
Lakini Bw Mutua alisema wafanyakazi wa afya ‘hawaufuata maadili’ kwa kutorejea kwenyw majukumuyao.
Alisema majinayaoyameondolewa katika orodha ya wafanyakazi wanaolipwa mshahara na si ‘waajiriwa wa serikali tena’
Dr Victor Ng'ani, mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Afya, wafamasia na wataalam wa meno alisema ulikuwa ni uamuzi wa ‘kizembe.’
Aliiambia BBC kuwa itakuwa vigumu kuwapata wafanyakazi mbadala kuziba nafasi ya miaka mingi ya watu wenye uzoefu na ujuzi wa kazi maalum.

bbcswahili

No comments:

Post a Comment