Friday 23 March 2012

WEMA NA JOKATE TENA


Stori; Joseph Shaluwa na Imelda Mtema
LILE tifu lililoanza kufutika taratibu kati ya warembo Wema  Sepetu na Jokate Mwegelo, limeibua mazito baada ya wawili hao, kila mmoja kwa nyakati tofauti kufunguka, mistari inayofuata ina kila kitu.
Awali Wema aliye Miss Tanzania mwaka 2006 na Jokate mshindi wa pili wa taji hilo, mwaka huohuo, alimtuhumu mwenzake kutoka kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wake, nguli wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’.
JOKATE PAAA!
Akizungumza kwenye Kipindi cha Ala za Roho katika Kituo cha Radio Clouds FM cha jijini Dar es Salaam, kinachoendeshwa na Loveness Malinzi ‘Diva’, pamoja na mambo mengine, Jokate alizungumzia suala la bifu lake na Wema na ukweli kuhusu tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
“Mimi sina tatizo na Wema, hayo mambo yalishapita na sitaki tena kuyazungumzia. Nilishamtafuta Wema na kukaa naye na kumweleza hali halisi. Nilimwambia asinihusishe kwenye mambo yao (na Diamond).
“Yule ni mwanaume wake, yeye ndiye mwenye mamlaka naye, kama anahisi chochote amuulize yeye, si mimi. Namheshimu sana Wema na namuombea maisha mazuri kama mwanamke mwenzangu,” alisema Jokate katika sehemu ya mahojiano na Diva.
Alipoulizwa kama aliwahi kutoka na Diamond, alijibu hivi: “Ni kwa nini mnamuonea mtoto wa watu? Sijatoka na Diamond.”

HASHEEM, CHID BENZ, AY, FA NDANI!
Diva alimwuliza kuhusu tetesi kuwa, aliwahi kutoka na mcheza kikapu bei mbaya katika ligi kuu ya mchezo huo huko Marekani (NBA), Hasheem Thabeet na kuachana naye, akakanusha.
“Mengi yanasemwa, lakini mimi ndiyo naujua ukweli. Hasheem amesemwa kuwa eti nilitoka naye, Chid Benz naye ametajwa, AY na hata MwanaFA. Sasa kama ni hivyo nitatoka na wangapi? Mimi kama Jokate, kiukweli huwa navutiwa zaidi na vipaji.
“Napenda sana vipaji vya wenzangu na mimi kuvumbua vyangu. Hao wote nimekuwa nao karibu kwa sababu hiyo, lakini watu wanasema nimetoka nao. Mfano AY nilifanya naye wimbo wa King and Queen, ni vipaji tu ndiyo vinanifanya niwe karibu na wavulana wengi, ingawa watu wanaweza kuzungumza chochote,” alisema.
WAUME ZA WATU
Swali lingine alilokumbana nalo katika kipindi hicho ni kuhusu skendo ya kutoka kimapenzi na waume za watu.
Akijibu swali hilo, Jokate alisema: “Naheshimu sana mume wa mtu. Ni kweli mimi kama msichana mrembo, wanaume wananitongoza, lakini ninapogundua kwamba ni wa mtu, nakaa naye mbali kabisa. Siwezi kufanya hivyo, huo ndiyo msimamo wangu.”
Akaongeza: “Wapo waume za watu wanaonisumbua, lakini kama nilivyokuambia, sipo tayari.”
AELEZA SIRI ZAKE ZA MAPENZI
Aidha, Jokate kwa mara ya kwanza alifunguka kuhusu siku yake ya kwanza kulala na mwanaume, alisema alikuwa na miaka 21 na kwamba mpaka sasa ametoka na uhusiano ‘seriously’ wawili bila kufafanua zaidi.
Hata hivyo, alisema kwa sasa hana mpenzi kwa kile alichokieleza kuwa anamsuburi mwenye sifa anazozihitaji ikiwemo mwenye ngozi yenye rangi ya ‘chokleti’, aliye tayari kumpa kipaumbele katika mambo yake.

WEMA AJIBU MAPIGO
Juzi, Jumatano, Ijumaa lilimvutia waya Wema na kumwuliza kuhusu kukutana na Jokate na kuzungumza naye ambapo aliruka vikali.
“Hatujawahi kukutana kuzungumzia kitu kama hicho na haiwezi kutokea. Kama alisema aliwahi kukutana na mimi tukamaliza hiyo ishu, atakuwa anadanganya, si kweli hata kidogo.
“Kuhusu yeye kutoka na Diamond, mbona kila mtu anajua ukweli? Tena siyo mara moja, mimi mwenyewe niliwashuhudia mara kadhaa, achilia mbali zile ambazo nilikuwa naambiwa na watu.”

chanzo:GPL

No comments:

Post a Comment