Thursday 11 August 2011

BAADA YA KIKOMBE LOLIONDO SASA KUNA KONDOO NA MAANDIKO YA QURAN



Inaovyoonekana hadithi ya kikombe cha babu imeeksipaya maana sasa tumepata hadithi ingine latest kuna kondoo kazaliwa na maandishi makuu matakatifu toka ktk quran!
ndio manaake nchi ya watu wazembe na wavivu kila siku watakujia na hadithi mpya mpya za kuendeleza uzembe wao na uvivu.
inasemekana kondoo huyu wa mama GRACE MASSAWE toka kilimanjaro amezaliwa na hayo maneno!(nani anajua kama wameandika wenyewe kwa rangi?)
ndio usanii kila mahali na hii hadithi imepokelewa kwa mikono miwili na wananchi,na sasa hivi ni gumzo kali la nchi?
kichekesho ni kwamba nchi iko katika matatizo kibao kiuchumi na kiutendaji raia wameshakata tamaa ya ufumbuzi wa matatizo yao sasa wanakimbilia katika imani.
viongozi watakatifu wanalijua hili ndio maana wako kimya wanaendelea kumega mkate wao kiulaini maana raia wako busy kujadili kikombe mara kondoo wenzetu kule mjengoni wanazidi kuchota posho na posho za vikao.
kuna pahala tunaenda sasa kila raia ameamua kuwa mbinafsi,ashughulikie matatizo yake mwenyewe sababu ukisubiri watendaji wao wako busy pia kushughulikia matumbo yao na familia zao.
inabidi tujiangalie sasa na kujiuliza maana kama wewe hapo kwa sasa unashughulikia mlo wako tu wa siku kwa mbinde bora liende,
katika miaka 20 ijayo hali itakuwaje kwa wanao!unapotafakari hili kumbuka pia kwamba nchi inauzwa kwa kasi ya ajabu tena kwa miaka 99,nani atakuwepo kipindi hicho cha miaka hiyo??

tujiulize kwa huu ujinga watanzania tulio nao sijui tunaenda wapi maana tunashindwa kuhoji haya mambo hivi sasa tumekuwa mabubu tusingoje wazungu waje watufanyie hiyo kazi ya kuhoji
madhara ya haya mambo tunayoyaona sasa yanafanyika ni dhahiri kwamba badala ya kuja kuenziwa na kizazi kijacho tukifa,tutakuja kutukanwa na hata kukojolewa huku tukiwa humo ndani makaburini kwa ajili ya huu uzembe tulionao sasa,maana tukumbuke ni watoto wetu na vitukuu ndio watakuja kuwa hawana chao
najiuliza maswali mengiii sana kwamba ni nini kifanyike tujiokoe maana tunakoelekea ni kubaya sio siri.

NIMEANDIKA HAYA KAMA MTZ WA KAWAIDA TU MSINICHUKIE KWA KUSEMA UKWELI

6 comments:

  1. YOU TALK SHIT MY FRIEND.I THINK YOU HATE MUSLIM

    ReplyDelete
  2. Huyo si kafiri ndio mana anazungumza upuuzi wake mbona k.s kaweka lkn akuzungumza upuuzi kama huwo.

    ReplyDelete
  3. ungemuuliza yule mgalatia mwemzako Grace Masawe kama kachora na rangi na anafaidika na nini kuchora,ukweli utabaki palepale hata kama unajaribu kupotosha.

    ReplyDelete
  4. Yaani watoa comment watatu hawa wanachuki binafsi na mwanablog. hata point yake hawakuiona wanaona anasema upuuzi tu. Sense mnayoweza kuielewa nini sasa ikiwa mwana blogg katoa point ya nguvu imewashinda mnakimbia udini. Isaackin achana nao usiwajibu wanajiexpose ufinyu wa kuelewa jambo zito uliloliweka mbele yetu. KUWA WATANZANIA TUKO FRUSTRATED TUNATAFUTA FARAJA KATIKA MAMBO YA LOLIONDO NA MBUZI. WAKATI VIONGOZI WANAKAZANA KUTUCHUNA. hiyo inawashinda nini kuelewa??? Nyie 3 hapo juu ndio mnapotosha.

    ReplyDelete
  5. punguzeni jazba,someni mada muelewe kabla ya kum-kaffir mtu nini tabu yenu

    bro wa GLOBEN tupo pamoja,najua we bado unaumia pale.pole sana

    ReplyDelete
  6. mambo ya globen ya nini tena jamani nawe ah! two rules - usijibu wala usiprovoke.

    ReplyDelete