Wednesday 3 August 2011

WASHIRIKI VODACOM MISS TANZANIA 2011 KUINGIA KAMBINI

LINO INTERNATIONAL AGENCY LIMITED
P.O. BOX. 53069 DAR ES SALAAM, TELEFAX :+255 22 2120201,
Corner of Samora & Mkwepu Street ,  MOBILE: +255 753 764156,   DAR ES SALAAM.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Lino Internation Agency chini ya Mkurugenzi wao Hashim Lundenga ambao ni waandaji wa mashindano ya urembo ya Vodacom Miss Tanzania wametangaza Jumla ya warembo thelathini (30) waliofanikiwa kupata nafasi ya kushiriki katika Mashindano ya Urembo ya Vodacom Miss Tanzania 2011.

Warembo hawa wamepatikana baada ya kupitia ngazi mbali mbali za Mashindano ya Vodacom Miss Tanzania katika ngazi za chini, ikiwa ni pamoja na Vitongoji, Wilaya na  Mikoa, na hatimaye ngazi ya Kanda, Jumla ya Kanda kumi na moja (11) zilishirikishwa katika Mashindano haya, alisema Lundenga.

Alisema kambi ya Mashindano haya ya “Vodacom Miss Tanzania 2011” inategemea kuanza siku ya Jumatatu ya tarehe 8 / 8 / 2011 jijini Dares Salaam.

Lundenga alitoa wito kwa washiriki wote waliochaguliwa kushiriki kwenye kambi hiyo kuripoti tarehe iliyotajwa hapo juu bila ya kukosa, katika ofisi za Miss Tanzania zilizopo mtaa wa Mkwepu saa 4.00 asubuhi.

Mkurugenzi huyo aliwataja warembo wanaotakiwa kufika kambini kuwa ni Chiaru Masonobo kutoka Dares Salaam, Zerulia Manoko, Maua Kimambo, Dalilah Ghalib, Christine Mwenegoha (kanda ya kati) Chritine William, Atu Daniel, Leyla Juma (Nyanja za juu kusini) Zubeda Seif,Stacey Alfred, Rose Hubert (kanda ya kaskazini) Husna Twalib, Cynthia Kimasha, Mwajab Juma (Kanda ya Temeke) Neema Mtitu, Weirungu David (Open University) Glory Lory, Blessing Ngowi (Higher Learning) Loveness Flavian, Asha Salehe, Mariaclara Mathayo, (Kanda ya Mashariki) Trace Sospeter, Irene Karugaba, Glory Samwel (Kanda ya Ziwa) Stella Mbuge, Husna Maulid, Hamisa Hussein (Kanda ya Kinondoni) Salha Israel, Alexia Willims, Jenifer Kakolaki (Ilala)

Nae Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania Bw.George Rwehumbiza alisema kampuni yake ipo tayari kuwapokea warembo kwani mwaka huu wamejiandaa vya kutosha na wanatarajia kuyaweka mashindano haya ya urembo kuwa ya kimataifa zaidi kuendana na silogani ya Vodacom isemayo “Kazi ni Kwako”akimaanisha maandalizi yote yako vizuri kazi kubwa ni ni kwa warembo wenyewe tu kujiweka sawa na ili baadae waje kuipeperusha bendera ya Taifa letu kimataifa siku za usoni.

Lundenga aliongeza kwa kusema iwapo itatokea mshiriki kushindwa kufika kwa wakati na tarehe iliyotajwa hapo juu basi mshiriki huyo atakuwa amejiondoa mwenyewe katika Mashindano haya na nafasi yake kupewa mshiriki mwingine.


No comments:

Post a Comment