Wednesday 23 November 2011

CHALZ BABA NA JAMES KIBOSHO KUTIMKA TWANGA



HABARI za chini ya kapeti zinazofukuta kama moto wa kifuu zinaeleza kwamba upo mpango wa wanamuziki wawili wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ Charles Gabriel ‘Chalz Baba’ na James Kibosho kutimka kundini humo, shuka na mistaari.

Habari kutoka kwa chanzo chetu zinasema kwamba, tayari mazungumzo ya awali kati ya wanamuziki hao na bendi moja inayokuja juu kwa sasa Bongo yameshafanyika na kinachosubiriwa ni kuwekana sawa kabla ya kuhamia rasmi.

“Kila kitu tayari, hakuna ubishi kuwa Chalz Baba na Kibosho lazima waondoke Twanga. Wameahidiwa donge nono, lazima waondoke,” alisema mtoa habari wetu akisisitiza jina lake lisichorwe gazetini.

Kama kawaida ya Risasi Mchanganyiko kutoa nafasi kwa mhusika ‘kubansi’, ndivyo lilivyofanya kwa Chalz Baba, ambaye hakukanusha habari hiyo badala yake aliishibisha.

Chalz Baba anafunguka: “Ni kweli ndugu yangu mchakato huo upo, kama watanitekelezea nilichowaambia siku ile kwenye kikao tulichokaa pale Movenpick (Hotel) basi dalili za kuachana na Twanga zipo wazi.”

Kwa upande wa Kibosho hakupatikana mara moja, lakini Chalz alisema: “Unajua waliponiita waliniambia kwamba wanahitaji na mpiga dramu, nikawashauri wamchukue Kibosho kwa kuwa ni mkali. Mambo yangu yakiwekwa sawa ni wazi 


chanzo;GPLkuwa nitakwenda naye.”

No comments:

Post a Comment