Thursday 3 November 2011

TCRA yasomesha watatu kwa Sh2.2bilioni

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imegoma kupitisha hesabu za Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), kutokana na ubadhirifu wa fedha za umma. Ubadhirifu huo uliobainika mbele ya kamati hiyo ni pamoja na mamlaka hiyo kutumia Sh2.2bilioni kuwasomesha wafanyakazi wake watatu nje ya nchi mwaka 2009/10.

Jumla ya Sh4.1bilioni zilitumika katika kipindi hicho kugharamia mafunzo. Hayo yalibainika Dar es Salaam jana wakati Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Jaji Mstaafu Buxton Chipeta na menejimenti yake walipofika mbele ya kamati hiyo kuhojiwa kuhusu hesabu zao.
“Tumezikataa hesabu hizi kuna matumizi makubwa ya fedha za umma yasiyozingatia kanuni za fedha,” alisema Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe. Alisema TCRA imekuwa ikimlipa mwenyekiti wa bodi na wajumbe wake Dola za Marekani 350 kila mmoja kwa mwezi, sawa na Sh600,000 hivyo kutumia jumla ya Dola 2,000 sawa na Sh3.4milioni kwa ajili ya mawasiliano, wakati wao si watendaji wa shughuli za kila siku za mamlaka hiyo.

Aidha, alisema wajumbe hao walinunuliwa katika mwaka huo wa fedha, simu za mkononi zenye thamani ya Dola za Marekani 600, sawa na Sh1 milioni kila mmoja.

“Wajumbe wa bodi hawastahili posho hizi na kuanzia sasa wasilipwe kwa sababu siyo watendaji wa shughuli za kila siku. Pia kwa nini wanalipwa kwa kutumia Dola badala ya Shilingi ya Tanzania?” alihoji Filikunjombe. Makamu Mwenyekiti wa POAC aliongeza kuwa mamlaka hiyo imetumia Sh36 milioni kuwalipa posho wafanyakazi saba wa idara ya uhasibu wanaofanya kazi katika muda wa ziada, huku wakifanya kazi za kawaida wanazopaswa kufanya katika muda wa kawaida.

“Hawa wanalipana mamilioni ya fedha kwa kufanya kazi ambazo waliajiriwa kuzifanya na wanalipwa mshahara! Huu ni ubadhirifu,” alisema Filikunjombe.

Kamati hiyo pia ilibaini matumizi makubwa ya fedha katika ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam. Alisema licha ya mshauri wa mamlaka hiyo kukadiria gharama za jengo hilo kuwa Sh27 bilioni, hadi sasa kiasi kilicholipwa ni Sh45bilioni. Kamati pia imebaini matumizi ya Sh600milioni ambayo hayakufuata taratibu za zabuni ya ununuzi wa umma.
“Kiasi hicho kimetumika kununulia vifaa mbalimbali vya ofisi bila zabuni ya ununuzi kutangazwa jambo ambalo ni kinyume na sheria,” alisema Filikunjombe.

Alisema sheria inaruhusu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, kuidhinisha kiasi kisichozidi Sh50 milioni tu kwa mwaka.Akijibu hoja hizo, Mwanasheria wa TCRA, Elizabeth Nzagi alisema fedha za mawasiliano zimekuwa zikitolewa kwa wajumbe wa bodi ili kuwarahisishia mawasiliano baina yao na menejimenti.

Nzagi alisema mafunzo katika sekta ya mawasiliano ni gharama kubwa na hiyo ndiyo iliyofanya itumie Sh4.1 bilioni kwa mwaka. Hata hivyo, alisema si kweli kwamba Sh2.2 bilioni zilitumika kusomesha wafanyakazi watatu tu nje ya nchi, bali hayo ni makosa ya kihasibu.
Alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita, wafanyakazi wa idara ya uhasibu walilipwa Sh36 milioni za posho ya kufanya kazi katika muda wa ziada kutokana na uchache wa wafanyakazi.

“Tunatarajia kuajiri wafanyakazi wengine ili kazi hizo ziweze kufanywa katika muda wa kawaida,” alisema Nzagi.
Kuhusu gharama za ujenzi wa jengo la TCRA, Meneja Mawasiliano na Uhusiano, Innocent Mungy alisema inaweza kuwa juu kuliko makadirio kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi.

“Hakuna ubadhirifu katika ujenzi wa jengo lile hata uchunguzi ukifanywa kila kitu kiko wazi,” alisema.
Pia, Jaji Chipeta alisema hakuna ubadhirifu katika mamlaka hiyo akisema kilichojitokeza mbele ya kamati hiyo ni makosa ya kibinadamu katika utayarishaji wa hesabu zilizowasilishwa.

chanzo:mwananchi

No comments:

Post a Comment