Wednesday, 2 January 2013

DIAMOND APIGWA CHUPA NA MAYAI VISA KWENYE SHOO CLUB MAISHA

Diamond platinum amefungua mwaka vibaya baada ya show yake ya jana pale Maisha Club kumwendea ndivyo sivyo. Usiku wa Wasafi haukwenda kama ulivyokua umepangwa baada ya kutokea fujo kubwa.


Show hiyo ilianza saa saba na nusu na baada ya dakika chache za Diamond kwenye stage fujo zilianza baada ya kundi kubwa la vijana wasiojulikana kuanza kutukana watu, kurusha chupa na viti, kupigana na kupora vitu vya thamani kutoka kwa mashabiki wa Diamond. 

Chupa zilipoanza kurushwa kwenye stage ,moja ilimpata Diamond mkononi na nyingine ilimjeruhi mpiga picha wake Bestizo Mkononi. Kuona hivyo Diamond alishuka kwenye stage na kwenda kwenye chumba cha mapumziko mpaka fujo zilipotulizwa.


Vitu vya thamani kama cheni,pete na camera ya Bestizo ya This is Diamond iliporwa kwenye fujo hizo. Inasemekana Diamond na uongozi wa maisha ulipata taarifa kuhusu uwezekano wa fujo hizi kutokea na hatua zilifanyika kuweka usalama zaidi ila vijana hawa walikuwa wengi na ndio sababu ya show ya Diamond kuharibika.

chanzo:Mateja blog

No comments:

Post a Comment