Monday 23 April 2012

RAY AMBURUZA MANGE KORTINI



Mange Kimambi.
Vincent Kigosi ‘Ray’.



Na Mwandishi Wetu
JINSI kifo cha muigizaji supastaa Bongo, Steven Kanumba kilivyotokea, kilikuwa lazima kiibue mshindo mkubwa na ‘apdeti’ ni kwamba ‘godfather’ wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ atasimama kortini na mwanamke kiroporopo, Mange Kimambi.
Ray, amejiapiza kuwa lazima amfikishe Mange mahakamani kwa sababu ya kumzulia tuhuma kwamba yeye ndiye aliyehusika na kifo cha Kanumba.
Madai ya msingi kutoka kwa Ray ni kuwa Mange aliropoka kwenye blogu yake akimtaja godfather huyo wa Bongo Movie kwamba ndiye mhusika nambari moja wa kifo cha Kanumba.
Inadaiwa kuwa Mange alichapisha maneno kuwa aliyemuua Kanumba siyo muigizaji aliye mahabusu hivi sasa, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ila mhusika ni Ray.
Ijumaa iliyopita, Ray alimfungulia Mange mashtaka ya kumdhalilisha na kumchafulia jina kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay.
Kabla ya taarifa za polisi, Ray alinukuliwa kwenye tovuti moja nchini akibainisha kuwa hawezi kukaa kimya kwa sababu Mange amemchafua kwa kiasi kikubwa.
“Mimi huyo dada anayeitwa Mange Kimambi simjui na hili suala ni zito kwa hiyo siwezi kumuacha hivihivi, lazima nimfikishe mahakamani,” alisema Ray, akinukuliwa na tovuti hiyo.
Akizungumza na ripota wetu, Ray alisema kuwa mambo yote anayapeleka kisheria lakini hakusema ni lini shauri lake litafikishwa mahakamani.
Alisema: “Nilimuweka ndani leo (Ijumaa) lakini nasikia ameachiwa kwa dhamana. Nataka mashabiki wangu wajue hata iweje lazima nimfikishe makamani, siwezi kumuacha.
“Kanumba alikuwa mdogo wangu, nina historia ndefu na yeye. Tumeshirikiana mambo mengi kuliko mtu wa kawaida anavyoweza kukaa na kufikiri, sasa nawezaje kufanya njama ya kumuua mdogo wangu?
“Yote kwa yote, yeye ambaye anasema nimehusika, itabidi aithibitishie mahakama ni kwa namna gani nilihusika na kifo cha Kanumba.”
Wakati huo leo Lulu anatarajiwa kufikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa mara ya pili akikabiliwa na kesi ya kuhusishwa na kifo cha Kanumba.

chanzo: gpl

No comments:

Post a Comment