Friday 20 April 2012

WAHAMIAJI HARAMU BONGO!

haya wakati wengine tunaona kuishi bongo ni kama kituo cha polisi,huku kumbe kuna wenzetu wanatamani kuja bongo!kweli bongo hii hii watu wanakamatwa kila siku huko mikoani wakiwa wanasafirishwa au maporini wakitembea kuingia nchini.
sasa ndo utachoka kuna jamaa kibao toka somalia na ethiopia wanaingia kila kukicha hapa bongo wakati sie nae ndio tunatereeza kwenda huko kwingine kutafuta maisha maaana bongo hapalipi.

kwa swala hili mi nadhani imekuwa makosa hawa wazungu kuweka mipaka huku afrika,naonelea kama vile ingekua poa tu tunajizurulia kote afrika bila longolongo hii ya uhamiaji haramu,ingekua mtu ukitaka kwenda cameroon unajitwika kiroba chako huyoooo,ukitaka kumuona ghadaffi hewalaa,ukitaka kwenda south aah wewe tu hata kwa mugabe ingekua mchekea tu,
kichekesho sasa ni kwamba pamoja na vinchi vyetu hivi na njaa zake kali sana eti tunathubutu kumuita mwafrika mwenzetu muhamiaji haramu!
hii inaingia akilini kweli?kaja bongo kuchuma nini wakati sie wenyewe tunashindia uji wa muhogo!ingekua poa wangeachwa wajiingilie tu tugawane umasikini na sie tukienda huko makwao poa tu,haya mambo ulaya uitwe muhamiaji haramu(ole wako uitwe hivyo ulaya moto utauona) na hata afrika tuitane wahamiaji haramu mi naona sio fair kabisa bana.
hapa nimeelewa ndio maana mbongo akienda mtoni anajipiga kisonjo,maaana ukisema unatoka tanzania wakati wakimbizi wanakuja huko utaelewekaje?utaonekana tapeli tu na kupigwa chini kisha kipawa hiyoooo.

No comments:

Post a Comment