Saturday 7 April 2012

uchunguzi wa kifo cha kanumba waendelea


 Mwili wa Marehemu kanumba ukiingizwa chumba cha maiti Muhimbili usiku wa kuamkia leo
 Swahiba mkubwa wa Marehemu Kanumba, Ray Kigosi, akiusindikiza mwili ndani
Marafiki wa karibu. Picha na Spoti Starehe

Mamia ya waombolezaji wa kada zote wanamiminika nyumbani kwa msanii nyota aliyetutoka usiku wa kuamkia leo Steven Kanumba, ambako wakati mipango ya mazishi ikiendelea polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo chake chenye utata. Tamko rasmi halijatoka nasi tunaomboleza huku tukifuatia kwa karibu. Tuvute subira wadau.

Habari za awali ambazo kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Afande Kenyela amesema kuwa Kanumba alikuwa na kutoelewana kati yake na Mpenzi wake ambazo taarifa za awali zinasema waligombana na Kanumba alisukumwa na kugonga kichwa chini na mpenzi wake ambaye ametambuliwa kwa jina moja la Lulu.
Habari ambazo bado haijazithibitisha zinasema kuwa Kanumba alikuwa akioga ili atoke na ndipo aliposikia mpenzi wake akiongea na simu na mtu mwingine alipotoka kumuuliza ndipo mzozo kati yao ukaanza na katika hali ya kusumunana Kanumba alisukumwa akaanguka na kugonga kichwa chini.
Afande Kenyela alisema alipigiwa simu na ndugu wa Kanumba ambaye walikuwa wakiishi pamoja na Kanumba na walipofika Pale walikuta tayari ameshakata roho ila bado inasubiriwa ripoti ya daktari.
Kamanda Kenyela pia amesema kuwa mpenzi wak
e Maerehemu Kanumba anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi. Lulu ambaye naye anag’aa kwenye tasnia ya Filamu amekuwa akigonga vichwa vya habari vya magazeti ya “udaku” kutokana na skendo za mara kwa mara za mahusiano ya kimapenzi, ni majuzi tu mwanadada huyu ametimiza miaka 18 tangu kuzaliwa.


Aidha nyumbani kwa marehemu Sinza kumejaa ndugu jamaa na marafiki kiasi barabara ya kwenda Lion kupitia Madukani inapitika kwa taabu.
Kanumba ambaye alizaliwa mwaka 1984 amefanikiwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya movie za Tanzania si tu kwa Tanzania bali hata nje ya nchi pia. Kwa mashabiki wa filamu za kibongo Kanumba alikuwa ni namba moja na kwa kiasi kikubwa aliweza kuweka viwango kwani alikuwa anafaa kwa kila kona kuanzia kuigiza mpaka kuvaa na adamu ya maisha tofauti na ma Super Star wengine hivyo kuwavutia watu wa rika lote. Kanumba anamaliza kipindi chake cha miaka 28 akiwa ameacha kumbukumbu ambayo itaishi kwa muda mrefu.
 Chanzo: Spoti na Starehe 

No comments:

Post a Comment