Wednesday, 27 February 2013
VIROJA MADE IN SVERIGE!
haya haya leo tena tunawaletea vimbwanga vinavyoendelea hapa.
jana katika msako wa polis hapo mjini hotelini moja inayofahamika kwa kuuza makahaba.kimezuka jambo ambalo limekuwa kioja kinachoongelea sana hapa.hiyo ni pale polis katika kufanya msako wao na kufatilia kwa muda mrefu wakaamua wakatege mingo ili wamkamate kahaba japo mmoja tu akiwa na mteja wake.
polis hao wakatega mingo zao kwenye ngazi baada ya kuona kwa mbali katika microscope zao kwamba kuna mteja kaingia chumbani kwa kahaba.
baada ya kusubiri kwa muda mreefu sana mara jamaa akatoka ndani akiwa tayari kashakamuliwa wale wadudu.jamaa baada ya kutoka ndani ya room hamad polis wakamshtukiza"uko chini ya ulinzi"
yule bwana akanyosha mikono juu kuashiria kasalimu amri.
kichekesho na kiroja kinakuja wapi? ni pale polis walipotambulishana na kugundua kuwa kumbe jamaa waliyemkamata ndio hakimu ambaye walikuwa wanamtegemea sana kusimamia kesi kama hizo za makahaba.na hata hapo walipoenda kutega walikua wanasubiri wakikamilisha uchunguzi wampelekee yeye kesi.
sasa kesi ya nyani umpelekee nyani sijui itakuwaje.huyo bwana amekiri kwamba ndio alienda kufanya ngono na hajali,mke wake na watoto waliposikia akabwaga manyanga.wakili huyo hajutii kitendo hicho anasema tu ndio nimeenda na wamenikamata poa.
imebidi polis wamtafute hakimu mwingine ili asimamie kesi hiyo.
habari zaidi bofya HAPA
NB
KUANZIA SASA TUTAKUA NA KITENGO HIKI CHA VIROJA MADE IN HAPA HAPA,BADO TUNAENDELEA KULA NYAMA YA FARASI TUKIMALIZIA TUTAWAMWAGIA MASTORO HAPA INA LADHA GANI.
KAMA UNA KIROJA MDAU USISITE KUTUTUMIA
Tuesday, 26 February 2013
SAKATA LA POLIS KUULIZA VITAMBULISHO MITAANI LINAENDELEA
TASWIRA HII NIMEPIGA LEO HII MITAA YA MARIATORGET.NA HUYO ALIEKAMATWA HAKUWA DARK-SKINNED BALI MWEUPE MWENZAO ILA KWA MWONEKANO ATAKUA KISHOKA,ALIKUA HANA WASI WASI NA ANA UNIFORM,WAMEMUULIZA ID HAKUTOA WAKAMPIGA MASWALI MAWILI WAKASHTUKA ANALONGOFYA.HAPO HAPO WAKAMWAMBIA SHUKA KWENYE BASKELI(NIKAONA WANAMCHUKUA.
KUENI MAKINI BANDUGU,KIPAWA HAKUFAI UKISHUKA BILA ISSUE.
Dekula Band "Ngoma Ya Kilo"01-02/March/2013
Akadevu-Music present's;
Lady Neema,Bobo Sukari & Yaya Sella.
Dekula Band "Ngoma Ya Kilo"
Place:Lilla Wien"Little Nairobi"
Date:01-02/March/2013
Time:21.00-01.00
Addr:Swedenborgsg.20
Pendel:Södra Station
Monday, 25 February 2013
Rais Jakaya Kikwete Akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Mhe.Yousuf Bin Alawi bin Abdullahm
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akimkaribisha ikulu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufalme wa Oman Mhe.Yousuf bin Alawi bin Abdullah wakati waziri huyo alipomtembelea na kufanya naye Mazungumzo.
Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa Oman Mhe.Yousuf Bin Alawi bin Abdullah ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akimsindikiza Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufalme wa Oman Mhe.Yousuf bin Alawi bin Abdullah wakati waziri huyo alipomtembelea na kufanya naye Mazungumzo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Mhe.Yousuf Bin Alawi bin Abdullah(kushoto) baada ya kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine ni wajumbe waliofutana na Waziri huyo.
Picha na Freddy Maro-IKULU
Horsemeat found in Ikea meatballs in Czech Republic
Ikea has withdrawn meatballs from sale in 14 European countries after tests in the Czech Republic found traces of horsemeat in a batch made in Sweden.
Meatballs from the same batch had been sold in many states, including the UK, France and Portugal, the retailer said.Swiss food giant Nestle meanwhile said it had found horse DNA in meat from the Spanish supplier, Servocar.
The discoveries come as EU agriculture ministers meet for talks expected to focus on the growing horsemeat scandal.
Since the first horsemeat was discovered in frozen meals and burgers in the UK and Ireland last month, traces have been found in meat products across Europe.
'Testing like mad'
Ikea's announcement on Monday came after the Czech State Veterinary Administration said horsemeat had been found in 1kg (2.2lb) packs of meatballs manufactured in Sweden and shipped to the Czech Republic for sale in Ikea stores there.
A total of 760kg (1,675lb) of the meatballs have been intercepted and stopped from reaching Czech shelves, according to the Associated Press.
Horsemeat had also been found in beef burgers imported from Poland, the Czech State Veterinary Administration said.
In a posting on its Swedish Facebook page, Ikea first confirmed it was halting all sales of meatballs at its stores in the country.
Later, the company announced that meatballs from the affected batch of meatballs had also been sent to Ikea stores in Slovakia, Hungary, France, the UK, Portugal, the Netherlands, Belgium, Spain, Italy, Greece, Cyprus and the Republic of Ireland.
"We do not tolerate any other ingredients than the ones stipulated in our recipes or specifications, secured through set standards, certifications and product analysis by accredited laboratories," a statement said.
Also on Monday, the Spanish agriculture ministry announced that traces of horsemeat had been found in beef pasta meals produced by brands owned by Nestle.
A statement on the Swiss company's website said it was withdrawing six "La Cocinera" products and one "Buitoni" product from shops in Spain, and that it had halted all deliveries from the meat supplier, Servocar.
Nestle said testing continued across its products, a week after it announced that it was withdrawing two types of beef pasta meals from supermarkets in Italy and Spain which had been supplied by a company in Germany, H J Schypke.
A Nestle spokesman told the BBC the discovery of horsemeat in the products of a second supplier was not an indication that the problem was widespread across the company, but because "we are testing like mad".
'Concrete action'
The labelling of the origin of meat and the traceability of the products will be high on the agenda at the EU ministers' meeting.
Europe's food retailers depend on a complex network of brokers, cold stores and meat-cutting plants around the continent from which to source the ingredients wherever they are cheapest, says the BBC's Christian Fraser, in Paris.
Meat scandal
- In mid-January, Irish food inspectors announced they had found horsemeat in some burgers stocked by UK supermarket chains
- Subsequently, up to 100% horsemeat found in several ranges of prepared frozen food in Britain, France and Sweden
- Concerns that a drug used to treat horses, and which may be harmful to humans, could be in food chain
- Meat traced from France through Cyprus and the Netherlands to Romanian abattoirs
- Investigation suggests adulteration was not accidental but the work of a criminal conspiracy
The evidence of the past few weeks shows that national food safety authorities have failed to identify a problem in the supply chain over a significant period of time, he adds.
While the original agenda of the EU meeting included support for rural communities and the common fisheries policy, it is expected ministers will now try to come up with measures to tackle the horsemeat scandal.Those could include a pan-European labelling project for frozen food, a move which has the backing of France and Germany.
Paris and Berlin both want compulsory labelling and traceability.
UK Environment Secretary Owen Paterson said on Friday that he would "continue to insist on concrete, co-ordinated action right across Europe when I meet European agriculture ministers on Monday".
But a workable deal could be difficult, our correspondent says. The discovery of horsemeat comes in long, complex and poorly regulated supply chains in the meat industry.
At least a dozen countries are involved in the horsemeat affair, which implicates some of the biggest meat processors and food producers.
Italy joined the list on Saturday, reporting horsemeat in some lasagne products.
On Friday, Germany's consumer affairs ministry announced it had found traces of horse DNA in 67 of 830 food products tested.
Irish authorities on Friday suspended production at one processing plant after horsemeat was found labelled as beef.
bbc
Sunday, 24 February 2013
MTOTO HUYU KAPOTEA KAHIFADHIWA ANAYEMJUA APIGE NO HIYO 0714 229229
Jamani mtoto huyu kapotea ambaye anaye kujua kwake naomba anijulishe yuko home namba yetu ni 0714 229229 Kwa mawasiliano zaidi .... Jamani week mbili yuko kwetu tuwe wastahalabu atakae mjui apige simu .........
Saturday, 23 February 2013
TABIA ZA SIMU ZA KICHINA!
1.Ndege ikipita ,simu inaandika 1 missed call
2.Ukiwa karibu na lorry likawashwa kitu kinaandika "Charger Connected"
3. Battery inajaa baada ya dk 3 ....
4. Simu ina Tv,microwave,torch,kikata kucha,mswaki,kiberiti cha sigara
5. Unaweza andika Msg kwa "tooth pick"
6.kuna matatizo ya kimaandishi mfano Nokla,Blackderry,Samvang
7.Ukiingiza vocha zaidi ya 5,000 inakuuliza "are you serious??"
8.kukiwa hamna umeme inaandika "insert sim card"
9.ukipost status 1 facebook ina post 10 nyingine bila wewe kujua
10. Ukipita karibu na mchina uku bluetooth ikiwa on ,simu inaonesha new hardware found, please enter pairing code
by-jf member bujibuji
HAPPY BIRTHDAY MY SON MILTON!
Fundi magari
kama baba yake,nilitengeneza sana magari ya waya na vikopo enzi hizo mpaka kuitwa "mjapani"huwezi kuamini utotoni nilikua na yadi ya kuuza magari.gwala gwala nishazilamba sana.
busy kazini
nishaelewa kijana atakua nani hapo baadaye,maana dalili zinaonekana.ukiona mwanao anacheza sana sindimba na mahepe utotoni ujue huyo lazima atakua mganga wa kienyeji ohoo.
checking
"kapiteni"
milton "haya jamani mi ndo naondoka"
sisi wazazi kijijini"haya mwanetu wasalimiege huko mawinguni,ukimuona mungu simama umsalimie,umwambie tunampendaga sana na tunasali sana kanisani baba"
milton anajibu huku akicheka "ho ho hoo,haya ntamwambia"
hapo anawaza hawa wazee mafala kweli wanazani huko juu unamuona mungu duh.
ready to go!
kitu kinawashwa
misele
kisha huyooooo!
"HAPPY BIRTHDAY SON"
TAARIFA BAADA YA HABARI
KIJANA WETU MILTON ISAAC NASAAR Jr AMEFIKISHA MIAKA MIWILI SASA MUNGU ASHUKURIWE.NA KWAKWELI UKUBWA UNAANZA KUONEKANA MAANA SASA HATUWEZI TENA KUMLAZIMISHA KITU ASICHOTAKA ANAKWAMBIA HAPANA,SITAKI BLANK-OUT.NA INABIDI UMSIKILIZE,HABARI YA VIBOKO HUKU HAMNA KWAHIYO NDO HIVYOTENA.
DALILI NJEMA ZINAONEKANA VIZURI NYUMBANI NA HATA SHULE PIA WALIMU WANATOA CREDIT ZAO,HIVYO SINA WASI WASI KIJANA ATAKUA NA FUTURE NZURI TU.
SIE WAZAZI WAKE WENGINE TUMEKULIA UMAGANGANI,TANGU UNAZALIWA UNAKUA NI FULL KUIBA MBOGA,AU MICHEZO YETU ILE YA KUJIPIKILISHA BABA NA MAMA,MNAPIKA MCHANGA HUKU MKIJIPA MATUMAINI MNAPIKA WALI.FULL KUPULIZA MOTO WA KUNI MPAKA MACHOZI YANAWATOKA.MCHANGA UNAIVA TOKA LINI?MKITOKA HAPO MMEVIMBA MASHAVU UTAFIKIRI WAPIGA MATARUMBETA WA MARQUIS ORIJINO.
MKITOKA HAPO MNACHEZA KOMBOLELA KAMA UNAVYOJUA MWISHO WA KOMBOLELA UNAVYOKUWAGA.
MAGANGA MWINGINE UNAMKUTA BADO MTOTO ANAJIFUNZA KUTENGENEZA KOROBOI UNATEGEMEA ATAISHIA WAPI.NDO MAANA MPAKA LEO TUMEKUWA NA MAISHA YA KUUNGA UNGA KAMA KUCHEZA LOTTO.
NI KUSHUKURU MUNGU TU KWAMBA KATUWEZESHA TU,NA SASA HIVI NI JAMBO LA KUTIA MOYO KUONA WAZAZI HUKO NYUMBANI WANAKAZANA KWELI KUWAPELEKA VIJANA WAO SHULE ZA KUELEWEKA.
INGAWA NI WALE WENYE KIPATO CHA JUU,HAWA WENGINE WASIO NA KIPATO BADO SHULE ZAO NI ZILE ZILE ZA KATA, MWALIMU ANALETA VISHETI NA ASKLIMU SAA NGAPI ANA MUDA WA KUFUNDISHA.
SHULE MNAAMBIWA MUENDE NA MAJEMBE.KIPINDI CHA MAPUMZIKO MNAENDA KULIMA MCHICHA KWENYE SHAMBA LA MWALIMU,MWEEH!
WEEK END NJEMA WADAU
Friday, 22 February 2013
TAHADHARI POLIS KUULIZA ID-CARD NDANI YA TRENI
KUMEKUWA NA MATUKIO MENGI YA WATU (HASA WAHAMIAJI)KULALAMIKA KWAMBA SASA WAKIWA NJIANI AMA NDANI YA TRENI WAMEKUWA WAKIKUTANA NA POLIS NA KUULIZWA VITAMBULISHO.HILI SWALA LIMEKUWA KUBWA KIASI SASA LIMEFIKA KATIKA VYOMBO VYA HABARI.
SIJAWAHI KUKUTANA NA HIYO SITUATION LAKINI KUNA SIKU NILIWAHI KUSHUHUDIA WABONGO WAWILI WAKIWA WAMEKAMATWA NA POLIS NDANI YA TUNNELBANA WAKIULIZWA VITAMBULISHO,NILIPOWAULIZA WAKASEMA NI SWALA LA TICKET LAKINI HATA KAMA NI TICKET NIKASHANGAA IWEJE WAJE POLIS KUWAFATILIA BADALA YA MAVAKT WA KAWAIDA HAWA TUNAWAONA HUMO KILA SIKU.
PIA SIKU ZA HIVI KARIBUNI NIMEKUWA NIKIONA POLIS WENGI HUMO NDANI YA TUNNELBANA NA MA-TORG NIKAJUA WAKO KATIKA MINGLE ZAO ZA KILA SIKU.POLIS WAKIULIZWA WAMEDAI KWAMBA WAO WANAFUATA ODDER TU YA KUFATILIA ILLEGAR IMMIGRANT KWA HIYO WAKO KAZINI.
HIVYO HALI HALISI NDIO HIYO JAMANI KUWENI WAANGALIFU.
Sweden to keep immigrant kids in school
The government wants to make sure young immigrants keep up their studies by legally requiring them to stay in school until they reach 18, while also pumping funds into Swedish-language courses.
Education and Integration Ministers Jan Björklund and Erik Ullenhag proposed on Thursday that children who are older than twelve when they arrive in Sweden should have to keep studying until they are 18.
At present, Swedish children are bound by law to go to school until the year they turn 16, in practice finishing compulsory education. Attending high school is optional.
Björklund first hinted at lengthening compulsory schooling for newly-arrived children last autumn, as the government presented its annual budget.
At the time, he said that foreign-born children's academic performance had deteriorated in recent years, partly due to the surge of underage asylum seekers from Afghanistan and Somalia, whose education levels had suffered due to years of wars.
In addition, immigrant children were generally older than their Swedish-born peers when they enrolled in school in Sweden.
A proposed 30 million kronor ($4.7 million) per year would add three more hours of Swedish-language instruction per week for the first four terms that the children are enrolled in school.
The proposal also called for newly arrived children to start studying as soon as possible, rather than languishing in orientation courses that can stretch up to one year.
Björklund estimated that the changes would affect around 3,000 students in every grade.
TT/The Local/dl
At present, Swedish children are bound by law to go to school until the year they turn 16, in practice finishing compulsory education. Attending high school is optional.
Björklund first hinted at lengthening compulsory schooling for newly-arrived children last autumn, as the government presented its annual budget.
At the time, he said that foreign-born children's academic performance had deteriorated in recent years, partly due to the surge of underage asylum seekers from Afghanistan and Somalia, whose education levels had suffered due to years of wars.
In addition, immigrant children were generally older than their Swedish-born peers when they enrolled in school in Sweden.
A proposed 30 million kronor ($4.7 million) per year would add three more hours of Swedish-language instruction per week for the first four terms that the children are enrolled in school.
The proposal also called for newly arrived children to start studying as soon as possible, rather than languishing in orientation courses that can stretch up to one year.
Björklund estimated that the changes would affect around 3,000 students in every grade.
TT/The Local/dl
Thursday, 21 February 2013
RATIBA SIKU YA UMOJA WA WATANZANIA SWEDEN
RATIBA
Tanzaniska
Riksförbundet programmet 1 Årsjubileum den 23/2
Kl 15.00–16.30 Årsmötet
16.30–16.45 Berättelse om föreningens framtid
fika pausen
16.45–17.20 Frågesport
17.20–18.00
Annonserar vinare i frågesport
18.00–21.00 Middag och Mingel
Riksförbundet
önskar er alla en trevlig dag!
Watuhumiwa mauaji ya Padri Mushi wakamatwa
*Wadaiwa kusafiri kwa Jahazi kutoka Z’bar hadi Mombasa
*Wanaswa katika usafiri wa gari wakielekea mjini Nairobi
MAKACHERO wa Jeshi la Polisi nchini wamewatia mbaroni vijana watatu wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Padri Everist Mushi (55) wa Kanisa Katoliki mjini Zanzibar.
Watuhumiwa hao wamekamatwa mjini Nairobi, Kenya kutokana na ushirikiano wa Jeshi la Polisi la Tanzania na Polisi wa Kenya kwa mwamvuli wa Shirikisho la Polisi wa Kimataifa (Interpol).
Habari za kuaminika kutoka Nairobi, Kenya zimesema kuwa watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa, walitiwa nguvuni juzi mjini humo walipowasili wakitokea Mombasa, mashariki mwa nchi hiyo.
Watuhumiwa hao ambao walikuwa wakiingia katika maficho kukwepa mkono wa dola, wanadaiwa kutumia jahazi kusafiria kutoka Zanzibar hadi Mombasa, Kenya kabla ya kusafiri kwa magari hadi Nairobi ambako walitiwa nguvuni.
“Tuliwakamata wakitokea Mombasa kwa basi kuja Nairobi. Baada ya kuwakamata tuliwafanyia mahojiano na baadaye tuliwakabidhi kwa polisi Tanzania,” kilisema chanzo chetu.
Tayari watuhumiwa hao ambao walikuwa wakifuatiliwa kwa karibu wamerejeshwa nchini kuunganishwa na watuhumiwa wengine waliopo katika mtandao huo.
Watuhumiwa hao walisafirishwa jana kwa magari kutoka Kenya kupitia mpakani Namanga wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na ushirikiano wa karibu wa majeshi ya polisi kwa ukanda wa nchi za Afrika Mashariki kwa mwamvuli wa Polisi wa Kimataifa (Interpol).
Watuhumiwa hao walitarajiwa kuwasili Dar es Salaam jana kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kuunganishwa na wenzao wengine kujibu tuhuma za mauaji zinazowakabili.
Alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusiana na kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali alisema hana taarifa zozote za kukamatwa kwa watuhumiwa waliohusika na mauaji ya Padri Mushi huko Kenya.
“Mimi sina taarifa zozote kama kuna watu waliokamatwa Kenya ambao wanahusishwa na mauaji ya Padri Mushi, lakini juhudi zetu za uchunguzi zinaendelea.
“Ninanchofahamu mimi ni kwamba wapo watuhumiwa ambao tunaendelea kuwahoji juu ya mauaji haya lakini sina taarifa za kukamatwa kwa watuhumiwa wengine nchini Kenya,” alisema.
Alipoulizwa iwapo kuna taarifa zozote ambazo zimefikishwa Interpol kwa msaada zaidi, Kamishna Mussa alisema: “Suala la wahalifu kuvuka mipaka inawezekana siwezi kukataa maana hawa ni binadamu.
“Lakini kuamini kuwa wanaweza kuvuka mipaka ni suala moja na suala la pili ni uchunguzi… Polisi haifanyi kazi kwa hisia tu tunajiridhisha kwa kufanya uchunguzi,” alisema.
Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein jana aliongoza mamia ya wananchi katika mazishi ya Padri Evarist Mushi katika eneo la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mazishi hayo yalihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini, mabalozi , wawakilishi, wabunge na viongozi wa vyama vya siasa kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.
Mapema asubuhi jana, Dk. Shein alitoa salamu za mwisho kwa Padri Mushi huko katika kanisa la Minaramiwili mjini Zanzibar.
Sala ya mazishi kanisani hapo iliongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo na ibada ya mazishi huko Kitope iliongozwa na Mhashamu Baba Askofu Antoni Banzi ambaye ni Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga.
Akitoa salamu za Serikali katika mazishi hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud alisema Serikali imesikitishwa na kifo cha kiongozi huyo wa dini na kwamba ni huo ni msiba mkubwa kwa taifa.
Waziri Aboud aliwaomba wanafamilia wa marehemu na waumini wa dini ya Kikiristo kuwa watulivu na wastahamilivu katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo ya kiongozi huyo.
Alimuelezea Padri Mushi kuwa alikuwa kiongozi aliyehubiri upendo, umoja na amani miongoni mwa waumini na wananchi wote wa Zanzibar na kuhimiza maadili mema hivyo kumuenzi kwa kumuombea maisha mema ya milele.
Nazo salamu za familia zilitolewa na Fransis Mushi na kutoa shukurani kwa niaba ya familia kwa ushirikiano mkubwa waliyoyapata katika msiba huo tokea siku ya tukio la mauaji ya Padri huyo hadi jana alipolazwa katika nyumba yake ya milele.
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Zanzibar Augostino Shao alieleza kusikitishwa na msiba huo na kumuomea marehemu amani ya milele.
Padri Mushi alizaliwa Juni 15, 1957 katika kijiji cha Uru Kimanganuni katika Mkoa wa Kilimanjaro na baada ya kumaliza elimu ya juu ya Sekondari mwaka 1976, alijiunga na Seminari Kuu Kibosho ambako alipata elimu ya Falsafa kati ya mwaka 1978 na 1979.
Mwaka 1980 alijiunga na Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo, Kipalapala mkoani Tabora alipopata elimu ya dini (Theology) hadi mwaka 1982.
Mwaka 1984 alirudi Kipalapala mkoani Tabora kuendelea na masomo na mwaka huo huo alipata Daraja la Ushemasi katika Parokia ya Bikira Maria wa Rosari Kitope Zanzibar.
Katika maisha yake ya Upadri alishika vyeo mbalimbali ikiwamo Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Rozari Kitope mwaka 1985, Paroko wa Parokia ya Moyo safi wa Maria wa Wete Pemba na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Antoni wa Padua Machui.
Padri Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 17 Mtoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar, na watu wasiojulikana.
chanzo-mtanzania
Wednesday, 20 February 2013
KATIBU MKUU WA BARAZA LA MITIHANI ADAI CLOUDS FM IMECHANGIA UANDIKAJI WA MATUSI KWENYE MTIHANI YA FORM 4 MWAKA HUU...!!!
Katibu mkuu wa baraza la mitihani la taifa, Bi Joyce Ndalichako, amekilaumu kituo cha Radio cha Clouds FM kuwa kilimpa promotion kijana aliendika matusi na "Bongo Flavor" katika mtihani wake wa Kidato cha Nne Mwaka jana kwa kumfanyia interview katika moja ya vipindi vyake.
Katibu mkuu huyo amedai kuwa hatua hiyo ya Clouds FM imechangia uandikaji wa matusi kwa watahaniwa wa mwaka huu.
Hata hivyo, watangazaji wa kituo hicho wamepinga vikali kauli hiyo na badala yake wamemtaka katibu mkuu huyo atoe sababu za kisayansi za kufeli kwa wanafunzi.
Source: Clouds FM asubuhi ya leo.
MTUHUMIWA WA MAUAJI ANAPOJIPELEKA POLISI NA KUAMBIWA TUMEFUNGA NJOO KESHO!
wahenga walisema ukistaajabu ya firauni utayaona ya musa,hiyo ilidhihirika hapa sweden maana kuna visa ambavyo ni made in hapa hapa vinachekesha kama sio kusikitisha.
wiki hii kumekuwa na matukio kadhaa ya kushangaza
1.ni pale vibaka walipoenda kuvamia duka la saa kwa nia ya kuiba huku wakiwa hawana silaha yoyote zaidi ya kujivisha sox usoni.ndio maana hapa ni kujaribujaribu tu,wameona wenzao wanaweka bag nje na kuandika bomb na wanaondoka na mali kibao huku polis wakiogopa kusogea kwanini na wao wasijaribu.mara hii vijana hao waliishia mikononi mwa polis baada ya kukamatwa kama kuku wanaoumwa mdondo.hongera hapo kwa polis wa sweden.
2ni pale ilipokuja gundulika kwamba kumbe yule gaidi aliyetaka kulipua mamia ya watu hapo central station mwaka 2010 alikuwa siku zote za maisha yake anaishi kwa kufadhiliwa na pesa za serikali yasweden za msaada wa wanafunzi.mpaka siku anajilipua huyu bwana alikua na deni la zaidi ya koronar 750,000/=.na inasemekana siku mbili tu kabla ya kujilipua na jaribio lake kuua watu kushindwa.walikua wamemtumia tena 57,000/= koronar.thanx kwa serekali ya kiswede.
3.kubwa kuliko ni hii ambapo jamaa mmoja huko goteborg amekuwa wanted baada ya kumpiga risasi mmoja wa viongozi wa vikundi vya mafia huko.huyo bwana baada ya kuishi kwa kujificha ficha kwa muda mrefu akaamua ajipeleke polisi mwenyewe akashtakiwe.kufika polisi polisi wakamjibu kwamba "e bwana sisi tumefunga bana tunafanya marekebisho njoo kesho".jamaaa akajiondokea zake,baada ya siku 2-3 huyu bwana alipokutana na waandishi wa habari na kukutwa akizurula mitaani alipoulizwa akasema "mabwege wale,nimejipeleka wanasema wamefunga kituo mpaka kesho.mwandishi alipomwambia sasa si wamefungua uende akajibu"nani aende!?mi mwenyewe nshaghairi kufungwa"
haya habari ndio hizo nawahi box
Tuesday, 19 February 2013
KANISA LINGINE LACHOMWA MOTO ZANZIBAR
WAKATI Watanzania wakiendelea kutafakari tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Padre Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoriki Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadaye kulichoma moto Kanisa la Walokole la Shaloom lililoko eneo la Kiyanga kwa Sheha mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, ACP Augostine Olomi, amesema leo kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 9.30 usiku. Amesema moto huo ulizuka mara baada ya kikundi cha watu watatu kuonekana wakipita njia karibu na kanisa hilo na baada ya muda mlinzi wa kanisa hilo alisikia kanisa likishambuliwa kwa mawe juu ya makapaa.
Amesema baada ya mlinzi huyo kubaini kuwepo kwa hatari, alilazimika kukimbia kwenda kujificha lakini huku akiangalia kwa mbali kinachoendelea. Kamanda Olomi amesema kuwa wakati mlinzi huyo akiwa amejibanza mafichoni huku akiangalia kinachotokea, mara aliona moto ukiwaka ndani ya kanisa na ndipo alipopiga simu kwa kiongozi wa kanisa hilo naye kuwajulisha Polisi.
Amesema Polisi walipofika hapo walisaidiana na wananchi kuuzima moto huo lakini wakati huo tayari ulishateketeza thamani za kanisa hilo na vitu vingine vilivyokuwa kanisani hapo. Kamanda Olomi amesema moto huo ungeweza kusababisha athali kubwa kama usingedhibitiwa mapema.
Hata hivyo amesema uimara wa dali lililotengenezwa kwa Gibsam kumesaidia kuunusuru moto huo kuunguza mapaa na kuliteketeza kabisa kanisa hilo. Amesema wakati uongozi wa kanisa hilo ukifanya tathimini ya harasa iliyopatikana kutokana na moto huo, Jeshi la Polisi limeanza kuwasaka washukiwa kwa kutafuta taarifa kwa raia wema na bado hakuna mtu ama watu waliokamatwa kuhusika na tukio hilo.
Hata hivyo Kamanda Olomi amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii, wataanza utaratibu wa kuyalinda makanisa yote ili kuzuia matishio mengine kama hayo.
MAMBO YA SKYLIGHT BAND NDANI YA THAI VILLAGE
Pichani juu na chini ni Sony Masamba, Mary Lukas, na Joniko Flower wakitumbuiza mashabiki wa Skylight Band kwenye kiota cha Thai Village kinachowakusanya mashabiki kila Ijumaa ya wiki kutoka sehemu mbalimbali za jijini la Dar na vitongoji vyake.
Burudani ikiendelea.
Sony Masamba ndani ya hisia kali kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapata ile kitu roho inapenda.
Umeshawahi kusikia kipaji cha huyu dada…??? ni Aneth Kushaba AK 47 akiwajibika kazini, njoo Ijumaa moja ujionee mwenye.
Eric Ndalu akishow love na mdau.
Tumia pesa ikuzoeee. Vijana wanaojua kula bata mjini hawakosekani Kila Ijumaa wako na Skylight Band.
King Kif meno 32 yote nje anapoona wadada wazuri kama hawa.
Pichani juu na chini mashabiki wa Bendi inayoshika kasi mujini Skylight wakijimwaga na masebene yaliyokuwa yakiporomoshwa na Sony Masamba pamoja na Joniko Flower.
Joniko Flower akitoa buradani huku akisindikizwa na Aneth Kushaba AK47 pamoja na Mary Lukas.
Haki Ngowi (katikati) akishow some love na Fans wa Skylight Band Julio (kushoto) na Gideon (kulia).
Hayo yote ni mapenzi na Skylight Band….. Mdau akiwa ametweta jasho baada ya kusakata Sebene vilivyo akiona ashow love na dada zake.
Couples waliobamba kwenye Show ya Skylight Band wakishow love mbele ya Camera yetu…Karibuni tena.
Salma Yusuf akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band na mambo ya pwani (mduara) huku akipewa Sapoti na Mary Lukas sambamba na Sam Machozi.
Kijana David akianza kuonyesha woga wa kuzungushiwa nyonga huku akiwa amekaa.
Hapo sasa Kijana David akiwa ameelemewa: Warembo wa jijini Dar wakimpagawisha kijana na kumtoa jasho la pua.
Mwanadada akiwatoa jasho wanaume wawili wakati wa mduara shurti kuzungusha nyonga, haswa ukiwa nayo na dada yetu hapo amejaaliwa ndio raha ya kupitia unyago hiyo.
Hapo sasa twende kazi……..
Aneth Kushaba AK47 akishow love na Ceaser wa Clouds Tv pamoja na Dj Choka ambao ilikuwa mara yao ya kwanza kushuhudia Live Performance ya Skylight Band kwenye kiota cha Thai Village.
Bongo Flava nao ni moja wa mashabiki wa Skylight Band….Hemedy a.k.a PHD na Gelly wa Ryhmes walikuwepo kushow love na Skylight Band.
Dada Wendo all the way from Ughaibuni akishow love na mdau.
Joniko Flowe wa Skylight Band na fans wake.
Joniko Flower, Hemedy pamoja na Gelly wa Rhymes wakishow some love.Chanzo:
moeblog
Subscribe to:
Posts (Atom)