Friday, 31 December 2010

Jokate mwegelo mrembo wetu wa kufungia na kufungulia mwaka


miss jokate
sijawahi kumuweka huyu mrembo wetu hapa Hata siku moja.ni mrembo ambaye mimi binafsi Namu-admire kwa Kila kitu.kitabia,urembo,mavazi huwa Ananivutia sana kwa kila jambo kati ya warembo wengi bongo.nisiseme sana nimeamua ghafla kuweka post hii ya mwisho kufungia mwaka ya jokate mwegelo.nikirudi mwaka mpya nafungua na post nyingine ya jokate vilevile yenye ujazo kadhaa.karibuni kwa maoni yanayojenga sio unaa na kupakaziana,maoni mabovu kaa nayo tu mfukoni ukanywee bia hapa hatuyahitaji.yanayojenga yanakaribishwa.

ICE BLACK MAGIC IN LONDON 1-1-2011

new year bongomovie"HONEYMOON-2"enjoy

PART 1-3

PART 2-3 PART 3-3

karibuni tena wadau tunaendelea kupata uhondo wetu wa movie toka mitaa ya nyumbani bongo,niliahidi kuweka hii party two jumamosi iliyopita lakini nilizidiwa kidogo na mambo ya sikukuu na familia.by the way leo kitu iko hewani ni nyinyi tu na muda wenu kuicheki.haya tukiwa tumebakisha masaa kadhaa tuuone mwaka,ni muda mwingine wa kutafakari tumefanya nini kwa mwaka unaoisha?jibu najua kila mtu analo mwenyewe kwa kichwa.mie ndo naanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda kuumalizia mwaka huko mitaa ya town.tunaweza kugongana na msisite kupeana hi,maana sisi wote wamoja.

nawatakia HAPPY NEW YEAR 2011 wadau wangu wooote popote mlipo.

Barack Obama's Hawaii holiday 'costs at least £1 million'

obama family
U.S. President Barack Obama hits on the 17th fairway on the Klipper golf course on Marine Corps Base Hawaii while he is on Christmas vacation in Hawaii in Kailua, Hawaii....U.S. President Barack Obama hits on the 17th fairway on the Klipper golf course on Marine Corps Base Hawaii while he is on Christmas vacation in Hawaii in Kailua, Hawaii, December 23, 2010. REUTERS/Hugh Gentry (UNITED STATES - Tags: POLITICS)
obamas daughter

obama spend time with troops


The calculation of Mr Obama's holiday costs included $63,000 for his wife's early flight out, and $16,800 to house Secret Service agents and Navy Seals in beach front accommodation for two weeks.
There will be a further hotel bill estimated at $134,400 for 24 White House staff staying in the Moana Hotel at a rate of $400 a day.
The estimate, by the Hawaii Reporter, also included $250,000 for local police overtime, $1 million for the president's own round trip flight to Hawaii on Air Force One, and $10,000 for a local ambulance to accompany the presidential motorcade.
Additional costs such as staff meals, renting cars for White House staff, and travel costs for Secret Service agents travelling ahead of the president were not included, meaning the bill will probably be even higher.
The paper suggested the costs could have been kept down. It said the president could have stayed at a military base instead of the luxury 7,000 sq ft villa he has rented for $3,500 a day which has been dubbed the "Winter White House." Mr Obama is paying the rental himself.
The White House has insisted the cost of Mr Obama's holidays are in line with those of previous presidents.

source:the telegraph



Thursday, 30 December 2010

DUNIA INA MAMBO HII

Wakamatwa wakinadi nyeti za baba yao


JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limewakamata ndugu wawili wakitafuta soko la viungo vya binadamu walivyotarajia kupita kwa kumuua baba yao mzazi.Vijana hao walikamatwa wakitafuta soko hilo kwa mfanyabiashara maarufu wa mafuta katika
manispaa ya Songea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 6:00 usiku katika eneo la Msamala mjini hapa, kwenye ofisi ya kampuni moja ambayo inajishughulisha na uuzaji wa mafuta na usafirishaji wa abiria.

Alisema kuwa watu wawili ambao ni Mohamed Mohamed (25) na Hashim Yasin (25) wote wakazi wa Kijiji cha Hanga Monasteri wilayani Namtumbo, walifika kwenye ofisi hiyo na kumkuta mkurugenzi wa kampuni na  kumueleza kuwa wana viungo vya binadamu ambavyo wanataka kumuuzia.

Baada ya mazungumzo, watu hao walikubaliana kuwa viungo hivyo ni sehemu za siri za baba yao, ambazo zingeuzwa kwa sh. milioni sita na za kaka yao kwa sh. milioni tatu.

Baada ya makubaliano hayo, mkurugenzi huyo aliwasiliana na polisi ambao waliweka mtego na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao.

Kamanda Kamuhanda alisema kuwa watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa na polisi kuhusiana na madai hayo walikiri na kuwa walikuwa na mpango wa kwenda Tunduru kuwaua baba yao na kaka yao ili wafanikiwe kuchukua viungo hivyo na kuviuza kwa mfanyabishara huyo.

CHANZO:MAJIRA

models wa kufungia mwaka









haya heavy duty hizo"kula ushibe"

Swedes arrested over 'Muhammad cartoon plot'

soma habari hii ingia HAPA.
inasemekana jamaa walitaka kulipua headquarter ya kiwanda cha magazeti hapo denmark,lakini wamekamatwa sababu walikuwa wanafuatiliwa muda mrefu nyendo zao.haya si salama tena nchi za scandinavia

NEW YEAR PARTY AT SATRA SATURDAY 01 JAN 2011


kama mlivyoona mwanzo kulikuwa na party sollentuna lakini imeahirishwa badala yake itakuwepo siku hiyohiyo ukumbi sätra.karibuni

Tuesday, 28 December 2010

Serikali yasalimu amri kwa Dowans, SASA KUILIPA SH 185 BILIONI


HATIMAYE Serikali imesalimu amri kwa kukubali kulipa fidia ya Sh 185 bilioni kwa kampuni ya kufua umeme wa dharua ya Dowans Tanzania Ltd, huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema akisema kuwa "mjadala kuhusu suala hilo umefungwa rasmi". Ulipaji wa fidia hiyo unafuatia uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), Novemba 15, mwaka huu chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali, Jonathan Parker uliamuru Tanesco iilipe Dowans kiasi hicho cha fedha.

"Jopo la wasuluhishi limeamuru zaidi ya Sh36bilioni (dola za Marekani 24,168,343) na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya Sh 26bilioni (dola za Marekani 19,995,626) tangu Juni 15, 2010 hadi fidia hiyo itakapolipwa,’ ilieleza sehemu ya uamuzi huo.

Pia jopo hilo la wasuluhishi wa migogoro ya kibiashara liliamuru Sh60bilioni (sawa na dola za Kimarekani 39,935,765) na riba ya kiasi cha asilimia 7.5 ambayo ni sawa na Sh 55bilioni (dola za Marekani 36,705,013.94) zilipwe kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.

Jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi na za utawala Sh1bilioni (dola za Marekani 750,000) kwa wasuluhishi wa ICC zinatakiwa zilipwe na pande zote husika yaani Tanesco na Dowans.

"Tanesco wanatakiwa kumlipa mdai (mlalamikaji) Sh3bilioni (dola 1,708, 521) ikiwa ni gharama za uendeshaji wa kesi na gharama zingine na kwamba madai mengine yaliyotolewa na pande zote katika kesi hiyo yanatupwa.

Awali baada ya uamuzi huo kufikiwa, Tanesco ilionyesha nia kwamba ingechukua hatua za kukata rufaa, lakini Jaji Werema aliliambia Mwananchi jana katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam kuwa hakuna haja ya suala hilo kukatiwa rufaa, hivyo kuyeyusha ndoto hizo za Tanesco.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, William Mhando katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari wiki mbili zilizopita alisema shirika lake lingeweza kutoa tamko kuhusu hatua za kuchukua kuhusu uamuzi wa ICC, lakani akaweka wazi kuwa walikuwa wakisubiri uamuzi huo kusajiliwa rasmi katika Mahakama Kuu nchini.

Hata hivyo,  kutokana na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, sasa ni rasmi kwamba hakutakuwa na hatua zozote za kisheria dhidi ya uamuzi wa ICC na badala yake Tanesco watatakiwa kujipanga kuwalipa Dowans mabilioni hayo ya shilingi kama walivyoamriwa.

Taarifa za ndani ya Tanesco, zinasema kwamba shirika hilo limeanza kuweka fedha kwa ajili ya  malipo katika benki moja (jina tunalihifadhi kwa sasa) jijini Dar es Salaam

Akizungumza na Mwananchi baada ya hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu mpya, Mohamed Chande Othman jana, Jaji Werema alisema ameshamaliza kuisoma hukumu hiyo na kufanya uamuzi ambao tayari ameukabidhi kwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja kwa ajili ya hatua nyingine baada ya kuridhika nayo.
 “Mimi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali nimeisoma hukumu hiyo kwa makini na nimeridhika nayo kuwa iko sawa,” alisema Jaji Werema.
Alisema kwa maana hiyo, haoni haja ya kukata rufaa na kwamba licha ya kusikia baadhi ya watu wakijigamba kwamba wakipewa kesi hiyo wanaweza kushinda, amewaambia mawakili wa serikali kwamba asingependa kusikia uwepo wa mpango wowote wa kukodi mawakili kwa lengo la kuendelea na kesi hiyo.
“Kwa hukumu hii siwezi kusema tutalivalia njuga suala la Dowans maana kwa hukumu hii hata ukiivalia hiyo njuga itafikia mahalai njuga hizo zitakatika tu,” alisisitiza Jaji Werema.

Kauli ya Jaji Werema imekuja wakati wanaharakati, wananchi wa kawaida na baadhi ya viongozi wa serikali wakipinga waziwazi hukumu hiyo akiwemo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta aliyekaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa  kuilipa fidia Dowans "ni kuhujumu uchumi wa nchi".
Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa akiongoza vita dhidi ya ufisadi alikwenda mbali zaidi na kudai kwamba kuilipa Dowans ni mbinu chafu za watuhumiwa wa ufisadi ambao bado wana ajenda za kuingia Ikulu mwaka 2015.
Hata hivyo, katika mazungumzo yake jana, Jaji Werema alisema kwa mtu yeyote makini hawezi kupinga hukumu hiyo kwani mfumo wa uamuzi unaotumiwa na ICC hauwezi kutoa fursa ya kuwepo chochote cha kupinga.
Alisema wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo pande zote, yaani Tanesco na Dowans walimchagua msuluhishi wake na kwamba baada ya wasuluhishi hao kutoa uamuzi, ulipelekwa katika mahakama hiyo kwa ajili ya kuupitia na kuuthibisha.
Kuhusu hoja kwamba huenda upande mmoja ulitumia mbinu chafu katika kupata ushindi, Jaji Werema alisema msuluhishi anayeteuliwa na pande zinazohusika katika kesi si wakili wa upande wowote na kwamba jukumu lake ni kuangalia suala zima tu jinsi lilivyo na kutoa uamuzi wa haki.
“Hata  unapomteua mtu kuwa ‘Arbitrator’ (msuluhisi) si wakili wako, hivyo unaweza kumkataa. Kuna taratibu za kumkaba, lakini huwezi kumkataa kwa sababu hafuati mambo yako bali kama hafuati ‘ethics’ (maadili ya kazi),” alisema Jaji Werema na kuongeza;
“Kwanza arbitrator hapaswi kujua mambo yako na hupaswi kumweleza, hivyo upande mmoja ukijua kuwa umemweleza mambo yako una haki ya kumkataa,”.
Mwanasheria huyo Mkuu wa Serikali alieleza kushangazwa na kejeli na malalamiko yanayotolewa na watu mbalimbali juu ya uamuzi huo akidai kuwa hao wanaopiga kelele sasa wakipinga uamuzi huo ndio baadhi yao walikuwa wakipiga kelele kuishinikiza serikali kuvunja mkataba na Dowans.
Jaji huyo alisema kuwa kuna upotoshaji katika hukumu hiyo akidai kuwa kuna mambo mengine ambayo yamekuwa yakisemwa katika hukumu hiyo jinsi isivyo sahihi.
“Watu wamezungumza sana, nendeni mkaisome muone ile Dowans ni ya nani na imesajiliwa wapi, maana watu walitaka kupotosha kidogo,” alisema Jaji Werema.
Ingawa hakuweza kuainisha aina ya upotoshaji huo, lakini Jaji huyo alisema kwa mujibu wa rekodi, Dowans ilisajiliwa Costa Rica na kwamba inaonesha kuwa Rostama Aziz (Mbunge wa Igunga) alipewa nguvu ya kisheria tu.
Hivyo alitoa wito kwa Watanzania wote wanaoweza wausome kwanza uamuzi huo ili kuweza kujua hasa mfumo uliotumika katika usuluhishi, hadi kufikiwa kwa uamuzi wa Dowans kupewa haki ya kulipwa.

Tanesco inabeba mzigo wa kulipa gharama hizo wakati ambao nchi imekumbwa na mgawo wa umme untokana na kasoro mbalimbali katika mitambo ya kuzalishia nishati hiyo, sambamba na uamuzi wa kupandishwa kwa gharama za umeme ambao umelalamikiwa na wananchi.

source:mwananchi

HIVI HAYA MAMBO YATAENDELEA MPAKA LINI TANZANIA?

Monday, 27 December 2010

AMBULANCE!

BOBAN ARUDI BONGO TENA KWA MAZOEZI ZAIDI


haruna boban
Wazungu wamrudisha Boban Dar es Salaam

UONGOZI wa klabu ya Syrianska ya Sweden umemrejesha nyumbani kiungo wa zamani wa Gefle IF, Haruna Moshi ili ajifue zaidi kabla ya kupewa nafasi nyingine ya kufanya majaribio akiwa fiti.

Kocha Mkuu wa Syrianska, Ozcan Melkemichel ameliambia Championi Jumatatu kwamba, wamekubaliana na Boban pamoja na wakala wake, Damas Ndumbaro kuwa kiungo huyo anapaswa kujifua zaidi ili arejee nchini humo mwezi ujao.

“Lazima tufanye hivyo, benchi la ufundi limeona ni mchezaji mzuri. Lakini hakuwa na mazoezi ya kutosha wakati anakuja huku. Tumezungumza naye na ametueleza hakuwa anashiriki mashindano yoyote kwa kutokuwa na timu.

“Kwetu si kitu kibaya kwa kuwa kiuwezo tumeona yuko safi, sasa tutakuwa na mechi za kirafiki kuanzia Januari katikati.

Sasa watu wote wanaenda kwenye sikukuu na tunaona hatakuwa na nafasi nzuri ya kujifua hapa sababu ya hali ya hewa. Tumemtaka arudi kipindi hicho ili aweze kumalizia nafasi hiyo ya pili ya majaribio halafu tutatoa jibu,” alisema Melkemichel.

Boban tayari amerejea nchini na kueleza ingekuwa vigumu kwake kujifua vya kutosha akiwa nchini humo kutokana na baridi kali inayotokana na barafu kumwagika hadi kuzuia viwanja kutumika.

Awali, Boban alikuwa akiichezea Gefle IF ya Sweden, lakini aliamua kuvunja mkataba na kurejea nyumbani kabla ya kurudi tena nchini humo kwa ajili ya kufanya majaribio.

Baadhi ya timu za Sweden pia zimekuwa zikionyesha nia ya kumsajili, moja wapo ni GAIS ingawa, hapo awali kumekuwa na taarifa kwamba Boban hakuvutiwa nayo.

source:GPL
ushauri kiduchu kwa bwana boban,kama kweli anahitaji kucheza soka la kulipwa,ajitahidi kupiga zoezi ili akirudi tena hapa akubalike asajiliwe.inabidi akaze buti kweli,maana yaelekea hata yule agent wake ana moyo kweli kwa mafanikio ya boban na ndio maana anamtafutia timu mara kwa mara ajaribu.boban inabidi pia aelewe kwamba mafanikio hayaji siku moja ni mtihani na mitihani mpaka hapo unapo succeed,hii biashara ya nenda rudi nenda rudi inazidi kumuharibia,na usikute hawa syrianska wamemtosa baada ya kupewa feed-back ya tabia yake aliyoifanya alipokuwa gävle if.inabidi boban aelewe kwamba kile alichokifanya kule wale jamaa(gävle if) wamerekodi,na hawataficha wala kudanganya kuiambia timu yeyote iliyopo hapa inayokuhitaji yale uliyoyafanya ulipokuwa nao.mabaya au mazuri.hapo ndio mwenyewe utakumbuka nini ulifanya kibaya au kizuri na ambacho kinaweza kukuponza katika utafutaji wako wote.nahisi kabisa yawezekana nafasi ya wewe kuchezea syrianska ilikuwepo wazi na jamaa wameweka longolongo baada ya kuulizia file lako kule kwenye ile timu uliyopakaza.yawezekana wale wameeleza mambo yako yote na ndio maana wanakutosa kwa vijisababu visivyoeleweka.anyway niwewe mwenyewe unajua kinachoendelea.kama ni kweli sababu niliyotoa ndiyo iliyosababisha,basi tena mzee utafute uelekeo wa kwenda cheza nchi nyingine yeyote ulaya,maana kama ikiwa ni sweden tena lazima mwisho watarejea kuuliza tabia yako kule kwa timu uliyotaja umechezea  before(gävle) na wale wakiulizwa hawatachoka kumwaga utumbo wote uliofanya kule kama upo.ndio tunavyoishi hapa usishangae.mwisho hii ni tafakuri yangu tu,kama kweli issue ni mazoezi tu fanya kwa sana ukirudi tena uwaonyeshe kwamba wewe ni chaguo linalofaa.
nakutakia mafanikio mema katika kujenga maisha yako(sio taifa letu lililouzwa).
karibu tena sitoki-homu.

Sunday, 26 December 2010

Fake bomb empties Stockholm metro station

The Kungsträdsgården metro station in Stockholm was evacuated on Thursday night after a train driver alerted authorities to a suspicious package.
Authorities said on Friday that the suspicious package turned out to be a fake bomb.

Authorities were on high alert as the incident occurred less than two weeks after the country's first suicide bombing.

"It looked like a real bomb. Someone made it to frighten people," said Stockholm police spokesman Henrik Billestam.

Police described the packet as a object about the size of a milk carton, wrapped with silver adhesive tape with cables connected to a mobile phone.

On Thursday night police completely evacuated the Kungsträdsgården metro station and sent in deminers after a train driver alerted authorities to the possible threat.

The metro station is close to the seat of government in the Swedish capital.

Sweden has been on alert since December 11 when a suicide bomber, strongly believed to be Taimour Abdulwahab, first blew up his car and later himself near a crowded pedestrian street in central Stockholm.

He was carrying a cocktail of explosives and police suspect he may have left the crowd of Christmas shoppers due to a problem with the bombs when he mistakenly set off a small charge while standing in an empty side-street.

The bomber was the only person to die in the attack, but two people were slightly injured when his car exploded minutes earlier about 300 mtrs.
 
from :TL.

Saturday, 25 December 2010

HII KALI


Moroni. The Comoros has expelled a Tanzanian witch doctor suspected of having been hired to rig weekend elections with his magic, police said Thursday.
The juju man arrived in the Indian Ocean state two weeks ago and was repeatedly seen at the home of Mr Mohamed Abdoulhoihabi, the governor of the archipelago's main island of Grande Comore.

A senior police official who asked not to be named said the Tanzanian citizen was arrested on Tuesday on suspicion of working to influence the weekend's polls and was deported on Wednesday.

"He's a friend, he used to come for meals regularly," the governor's wife complained after enquiring about the Tanzanian's fate with the police.

"Nothing is clear or official. We are being told he is a crook but no warrant was issued... Internal security confirmed his arrest and simply told us that witchcraft was banned," she added.

Mr Abdoulhoihabi, once a close aide to Comoran President Ahmed Abdallah Sambi and now an opposition politician, will face a ruling party candidate as he attempts to retain his job tomorrow.

The federation is holding a national presidential ballot today as well as elections for the posts of governor on each of the three islands: Grande Comore, Anjouan and Moheli. (AFP)

source:mwananchi

Friday, 24 December 2010

christmass bongo movie"HONEY MOON-1"enjoy

NO 1-1 NO 1-2 NO 1-3 NO 1-4end ni sikukuu na nina kalikizo kidogo lakini nimeona itakuwa si njema kuwaacha hivihivi wadau,nimeweka hii muvi japo kupotezea time na sikukuu,hope mtaenjoy na nitaweka paty two yake kesho.week end njema.

NAWATAKIA CHRISTMAS NJEMA WADAU WOTE WA KIJIWE HIKI

Wednesday, 22 December 2010

JUMBO HOSTEL-A WORLD FIRST AEROPLANE HOTEL IN SWEDEN




Crammed into the 353 square metres of available space are 25 tiny rooms with space for 72 people overnight (along with a cafe) tended by uniformed cabin crew 24 hours a day.

muonekano wa nje wa dege hilo lililogeuzwa hotel




ukiingia unakutana na reception kama hotel za kawaida



kisha kuna siiting room kama hivi unavyoona



cockpit imegeuzwa room ya kulala utapenda


room nyingine kwa hivi
The jet, which was originally produced for Singapore Airlines, was taken out of service in 2002. It is held on a concrete foundation with the landing gear secured in steel cradles. <EM>Photo: Reuters</EM>

najua anasema valkommen ombod

Jumbo Hostels opened for business on Thursday, giving customers the chance to check in and sleep in a room that can best be described as cozy. <EM>Photo: Reuters</EM>

ndani kuna room 25 na zenye uwezo wa kuingiza watu 72

The world's first jumbo jet hostel is an actual jet-plane at Sweden's main airport outside Stockholm which has been converted into a 25-room guesthouse that sleeps as many as 72 people. <EM>Photo: Reuters</EM>

kwa wale mlio sweden najua hii kitu mshaiona pale mitaa ya arlanda labda mkadhani ni ndege inasubiri abiria ama inatengenezwa.noo hiyo ni hotel haswa.
kwa mnaohitaji kwenda chimbo"guest bubu"hiyo imepatikana,na kulala wala sio bei mbaya kurona yako 350 unapiga mboji hapo siku nzima bila kokoro.kuna cafe sema sehemu ya ulabu sidhani,ila unaweza kupitia systeme ukarekebisha maswala ukajichimbia humu pahali.




UHURU DAY KISTA

wadada walipendeza wakapendezeka vilevile
nikakutana na bloga mwingine(jalux.blogspot.com)

linda pia tulikua naye siku hiyo

linda friend

bwana mwelee mwelee alikua anaweka vitu taratibu


teh teh,jamaa yangu kila nikijitahidi kumpata vizuri picha ilikataa maana alikua kizani

mkamba alikuwepo pale chemba

ndugu zetu waliosababisha kule jikoni

ukapigwa mduara mwenyekiti mzuka ukapanda koti likawa zito akaingia uwanjani kama kawaida yake

aah mziki ukafunguliwa na sebene watu wakajimwaga

humphrey kwenye movement hapo utapenda

kisha kuna kapilau hapo pembeni,unajua ilipigwa nyimbo gani?zile oldies watu wakaanza kuvunja ama"brekn" kwa kimatumbi "mabreka"nyimbo ziliwakuna watu na tulivunja kweli,we angalia mikono hiyo ilivyokuwa inamuvuzishwa,bongo tuna kina maiko jakison wengi tu kumbe

hahaaa mukubwa akaona nyie mnatania ngoja niwaonyeshe hii inavyovunjwa.

sore picha zinafifia kamera yangu ilikua na kwikwi ya umeme si unajua mgao.

Tuesday, 21 December 2010

MIPAKAZO YA CHRISTMASS

SAFARI YA MWISHO YA ABUU SEMHANDO"BABA DIANA"


juu ni pikipiki aliyopata nayo ajali na chini ni wakati anazikwa
ABUU SEMHANDO ENZI ZAKE

sijui ni kutokana na mshtuko ama vipi,nilishindwa kumuongelea huyu mkongwe wa muziki aliyetutoka ghafla hapo jumamosi usiku kwa ajali.nilimfahamu abuu miaka hiyo 96-97,pale tulipokuwa tukifanya kazi pamoja pale new silent club(najua wengine mtasema huyu nae anamjua kila mtu).kipindi hicho ndio bendi ya diamond sound"wana ikibinda nkoy" ndio ilikuwa imeanzishwa tu na ilikuwa inazinduliwa rasmi.katika watu pekee waliokuwemo kwenye bendi hiyo ambao ni watz ni huyu bwana pekee aliyepata nafasi(maana wanamuziki wengine wote walikuwa wacongo).abuu alikuwa mtu mmoja charming na anayeongea na kila mtu hakuwa na maringo ya namna yeyote(maana wale wacongo ilikua tabu kipindi hicho)na alikua anaongea na kila mtu.nakumbuka baada ya kuzindua pale hatukukaa sana maana mie niliacha kazi baada ya uzinduzi tu wa bendi,nilishtukia ubabaishaji nikaanza nikawaacha wengine.abuu alivumilia sana na hiyo bendi sio siri,maana baada ya uzinduzi kulitokea na ubabaishaji wa hali ya juu wa mmiliki wa club hiyo.baada ya kutoka hapo nadhani abuu alikuwa ni mmoja kati ya wanamuziki waliojiengua diamond kisha kuunda dar musika iliyosimamiwa na marehemu choggy sly.dar musika haikudumu na ndio huyu bwana kuangukia twanga pepeta aliyodumu nayo mpaka mauti yalipomkuta.tukija kwenye utaalamu wa kuzikaanga hizo wanaita chipsi au mihogo,abuu alikua ni mmoja wa wataalam wakuu kabisa kwenye nyanja hiyo.nilikuwa mshabiki wa twanga mkereketwa hivyo naelewa huyu bwana alivyotia mchango wake katika ukuzi wa bendi ile pamoja na kusimamia nidhamu.jamaa alikua akikaa kwenye kiti sie wakereketwa ndio tunanyanyuka maana tunajua mzee mzima kaingia sasa ni muda wa kulipepeta twanga sebene.alikua akishaingia mzee pale nyuma,halafu kwenye tumba kuna mcd(naye alitoka diamond nilimkaribisha twanga siku ya kwanza anatambulishwa aliyoacha diamond sound kuhamia twanga) ,kuna yahaya mkango kwenye bass,kuna jojo jumanne kwenye solo,pale mbele unoz ulikua unamkuta jessica charles na luiza mbutu enzi hizo wakisindikizwa na amigolas(mwanamuziki wa kwanza kupendwa twanga,kabla hawajaanza kutunga nyimbo zao walikua wanaimba copy na amigolas alikua anaimba copy zote za kizaire),kinanda unamkuta profeshenee kibode mkambi,kushoto kuna ali choki,kulia kuna banza stone mwana masanja.timu ilikua imekamilika.tafuta nyimbo kama laitness,kisa cha mpemba na kuolewa.utajua naongelea nini.kweli tulikua tunatwanga kina mama wanapepeta huku BAPA linafanya kazi yake kichwani.ni kweli kwamba muhimili wa bendi umeondoka lakini najua twanga haitatetereka kwani kuna huyu kijana james kibosho  (niliona kipindi cha nyuma akielekezwa kuzipiga drums inavyotakiwa na baba diana) ambaye amechukua ukanda nayeye ni mtaalam mkali tu sasa hasa kwa hizi nyimbo za kisasa anajua kuzichapa hizo drums inavyotakiwa.najua hakijaharibika kitu.

MUNGU AMLAZE ABUU SEMHANDO PEMA PEPONI AMINA.