Friday 10 December 2010

KOFFI OLOMIDE&QUATIER LATIN ILIYOKUWA TISHIO




sanolaaa,eeeh sanolaaa(kerosene ndo kawachezesha watu hapa)

kama unaikumbuka hii timu ya quatier latin,kipindi hiki ndio ilikua bendi moja tishio sana congo D.R.C. sidhani kama congo kuna myuzishani yeyote alikua na sauti ya kusema yuko juu zaidi ya koffi,hii timu ilikua kamili maana humo ndani ulikua unamkuta ferre gola,fally,ipupa,soleir wanga,montana kamenga,bouro mpela,didier lacoste,ramazan fulutani,mirage sonic,felly tyson,lolla muana"digital".binda bass roberto carlos,fofo le collegion,bila kusahau pale kwenye kukaanga plate"chipsi"alikua mtaalam mwenyewe titina"al capone"huku nyuma unawakuta vijana wawili waliokuwa wakiwachezesha viuno watu "OBRIGADO" na "KEROSENE"pata picha mdau!aah mi mzee wa sebene nilishuhudia hii timu nzima ikifanya mambo pale diamond jubilee.sitasahau siku hiyo twanga waliingia na style zao za siku zote"sarakasi, mara kung-fu za kichina hu-haa"mradi fujo tu,walipoingia wenye kazi yao kwanza lilipigwa sebene la vyombo tu kwa dakika ishirini!kisha muziki ukazimwa MC siku hiyo(amina chifupa)akatutangazia kwamba vyombo tune haitoi kama jamaa wanavyotaka!hivyo tuwape nusu saa ya kurekebisha(kumbuka twanga wametupeleka na tune na sound hiyo)basi tukavumilia wazee wakaingia mtamboni kurekebisha,baada ya dk km 20 hivi wakazimua na solo fulani hivi kisha drum zikaitika mara bezi mara vitu hewani,likachapwa sebene lingine km dk 10,kisha likapokelewa na wanenguaji wakike,wakaingia wakatoa unoz la kufa mtu.waliporudi nyuma ikaingia timu niliyokutajia,nayo ikamwaga uno kiroho mbaya.ilichukua kama saa nzima bila kupumzishwa.kisha walipozima ndio akaingia mzee mwenyewe mopao mokonzi.kwakweli burudani ya siku hiyo sitaisahau kamwe.maana watu walichapwa sebene,nyimbo,unoz mwanzo mwisho. ilifika muda(saa 12 asubuhi) watu wanaondoka koffi anaita "vipi jamani mbona mnaenda"? watu wanajibu "aaah ngoja tukalale bana we unaimba tuu,kumekucha"ilikua balaa.

WEEK-END NJEMA

No comments:

Post a Comment