Thursday 30 December 2010

DUNIA INA MAMBO HII

Wakamatwa wakinadi nyeti za baba yao


JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limewakamata ndugu wawili wakitafuta soko la viungo vya binadamu walivyotarajia kupita kwa kumuua baba yao mzazi.Vijana hao walikamatwa wakitafuta soko hilo kwa mfanyabiashara maarufu wa mafuta katika
manispaa ya Songea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 6:00 usiku katika eneo la Msamala mjini hapa, kwenye ofisi ya kampuni moja ambayo inajishughulisha na uuzaji wa mafuta na usafirishaji wa abiria.

Alisema kuwa watu wawili ambao ni Mohamed Mohamed (25) na Hashim Yasin (25) wote wakazi wa Kijiji cha Hanga Monasteri wilayani Namtumbo, walifika kwenye ofisi hiyo na kumkuta mkurugenzi wa kampuni na  kumueleza kuwa wana viungo vya binadamu ambavyo wanataka kumuuzia.

Baada ya mazungumzo, watu hao walikubaliana kuwa viungo hivyo ni sehemu za siri za baba yao, ambazo zingeuzwa kwa sh. milioni sita na za kaka yao kwa sh. milioni tatu.

Baada ya makubaliano hayo, mkurugenzi huyo aliwasiliana na polisi ambao waliweka mtego na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao.

Kamanda Kamuhanda alisema kuwa watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa na polisi kuhusiana na madai hayo walikiri na kuwa walikuwa na mpango wa kwenda Tunduru kuwaua baba yao na kaka yao ili wafanikiwe kuchukua viungo hivyo na kuviuza kwa mfanyabishara huyo.

CHANZO:MAJIRA

No comments:

Post a Comment