Tuesday, 12 June 2012

BADI BAKULE(JOGOO LA SHAMBA) ARUDI TWANGA!


 
ilikua mshangao na raha kumuona Badi Bakule kule steji ya twanga hapo juzi,Badi ambaye alianzia kuwika akiwa na bendi ya tam tam hapo nyuma sambamba na muumin mwinjuma,juzi ameonekana akiwa live kwenye stage ya twanga mwanzo mwisho akiwa sambamba na wanamuziki wa bendi hiyo.
Badi bakule aliikacha tam tam na kuhamia T.O.T plus kabla ya kuikacha pia bendi hiyo na kuwa jogoo la shamba kweli baada ya kuhamia levert musica huko morogoro,
hii juzi ndio kaonekana kurudi mjini toka levert musika baada ya kula vumbi kidogo huko na kupigwa pigwa na upepo wa njaa ikabidi ampigie magoti maamaa Asha Baraka arudishwe kikosini.ok kijaana ndo hivyo karudi kwa shangwe lakini ajiandae maana game s hivi limechange maana hata siku hiyo nilimuona akiwa hana confidence yake ile ya mwanzo,ila namuaminia naona anajipanga upya kuja kivingine.maana kaikuta twanga tayari kuna vijana wapya wadogo wanapiga mzigo kama wamepagawa,masauti ya ukweli na seben la kufa mtu,
Diouf mwenyewe hivi sasa pale anachemka maana akiwepo ni kama hayupo hiyo sauti yake watu washaikava vizuri.anyway ntaendeleza hii storo maana nawahi mahali wadau


No comments:

Post a Comment