Thursday, 14 June 2012

MR NICE AGEUKIA UHUDUMU WA PUB


Nice Lucas Mkenda ‘Mr Nice’.
Na Issa Mnally
MWASISI wa staili ya Takeu Bongo, Nice Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ amewashangaza watu kwa kuonekana akiwahudumia wateja katika ‘pub’ mpya ya kisasa iitwayo Ako Labamba iliyopo Jumba la Maendeleo, Urafiki jijini Dar.
Paparazi wetu alimshuhudia msanii huyo hivi karibuni akitoa huduma hiyo sambamba na kuwakirimu wageni kwa tabasamu na kuwaonesha mahali pa kukaa kabla ya kuwauliza: “Niwahudumie nini? Vinywaji vyote vinapatikana hapa.”
Mnasa matukio wetu alipomuuliza msanii huyo kulikoni kuacha usanii na kuwafungulia watu ‘vyupa,’ na kuwahudumia msosi, Mr Nice alisema anafanya hivyo kwa nafasi yake ya ukurugenzi kwa lengo la kuboresha huduma.
“Mimi ni mmoja wa wakurugenzi wa pub hii, muulize yule ndugu pale,” Mr Nice alisema akimuonesha ‘mbaba’ aliyejitambulisha kwa jina la Anthony Gavin ambaye alikiri alichokisema Mr Nice.

source:GPL

No comments:

Post a Comment