Sunday 3 June 2012

TEAM TANZANIA YASHIRIKI RACE OF CURE

TEAM TANZANIA YASHIRIKI RACE OF CURE

Nancy G. Brinker mwanzilishi wa matembezi Susan G. Komen akiongea jambo kabla matembezi hayajaanza. Susan G. Komen ni dada yake aliyefariki na Saratani ya matiti. 
 
Mabango yaliyoandikwa kiswahili na Bendera ya Tanzania zikipepea kwenye matembezi hayo ya Susan G. Komen yaliyofanyikia Washington, DC, Nchini Marekani Jumamosi June 2, 2012 saa 2. asubuhi.
Team Tanzania ikiongozwa na mnusurika wa Saratani ya matiti Aunty Rehema (wapili toka kushoto)
 
Watanzania waliojumuka pamoja kwenye matembezi ya Susan G. Komen wakipata picha ya pamoja kwenye picha toka kushoto ni Aunty Asha, Afisa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani Asia Dachi na Salma Londa.
 Team Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza matembezi hayo.
Dada Mariam akiwa na mwanae Monica ambao hushiriki kila mwaka matembezi haya  wakitokea Durham, North Carolina.
 
Kikundi cha matarumbeka kikiwa njiani yanakopita matembezi hayo kikiendelea kuto burudani kwenye matembezi ya Susan G. Komen.
Watanzania wakiwa wenye furaha wakati wa matembezi hayo yaliyofanyikia Washington, DC Juamamosi June 2, 2012
 
Wahudumu wakujitolea wakisaidia kugawa maji ya kunywa kwa wanaohitaji.
 Timu Tanzania ikipata picha ya pamoja.
Juu na chini ni Ulinzi kila kona pamoja na magari ya kubebea wagonjwa kwa ajili ya tahadhali kama litatokea lolote.
Kikundi cha sarakasi kikitoa burudani kwa watembeaji hao.
 
Umati wa watu waliojitokeza kutoka kila pembe ya Marekani wakitembeamatembezi hayo ya Susan G. Komen yaliyofanyikia Washington, DC Jumamosi June 2, 2012.
Team Tanzania ikiwa imemaliza maili 3 kwenye matembezi hayo.
Team Tanzania ikiwa inakaribia kwenye Finish Line kumaliza matembezi ya maili 3.2 sawa na kilomita 5 yalyofanyikia Washington, DC Jumamosi June 2, 2012.
 
Team Tanzania ikipata picha ya pamoja baada ya kumaliza matembezi hayo.
 
 
picha na habari toka matukio-michuzi

No comments:

Post a Comment