Tuesday, 12 June 2012

MARCIO MAXIMO KUWASILI NCHINI JUMAPILI KUINOA YANGA


Marcio Maximo.
----
PRESS REALEASE N0 130
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
12/06/2012
Klabu ya Yanga inapenda kuwajulisha juu ya taarifa ya ujio wa Kocha Mkuu wa zamani wa timu ya Taifa,Taifa Stars, Marcio Maximo, ambaye alitarajiwa kuwasili leo hii, Sasa anatarajiwa kuwasili nchini Mwishoni mwa wiki hii.
Maximo ambaye tayari amekwishatumiwa tiketi ya safari ya kuja hapa nchini, ameshindwa kuwasili leo kutokana na Klabu yake anayofundisha ya Democrata F.C ya Mjini Rio de Jeneiro nchini Brazil kukabiliwa na mchezo mgumu siku ya Jumamosi wiki hii.
Marcio mara baada ya kuwasili nchini atafanya mazungumzo na Uongozi wa Klabu ya Yanga ikiwemo kusaini Mkataba na Klabu ya Yanga kabla ya kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho.
Kocha huyo kabla ya kuondoka nchini Brazil amewaahidi Wanachama na Wapenzi wa Klabu ya Yanga kuwa atafanya jitihada za kukiimarisha kikosi cha Mabingwa wa Soka wa Afrika Mashariki na Kati katika kuinua vipaji mbalimbali kupitia soka la Vijana wenye umri mdogo kwa ajili ya kupata wachezaji Bora.
Mambo mengine aliyoyapanga Kocha huyo ni pamoja na kuimarisha nidhamu kwa Wachezaji atakaokuwa akiwafundisha.
Marcio mara baada ya kuanza kibarua chake cha kukinoa kikosi hicho atakuwa na mtihani wa kwanza kwa kukabiliwa na michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Julai 23 hadi Agosti 7 Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment