Tuesday 12 June 2012

Miss Dar Inter College 2012 mazoezini



Na Mwandishi Wetu
WAKATI shindano la kumsaka  Miss Dar Intercollege 2012 likitarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) duka la vipodozi la Shear Illusions,pamoja na mbunifu maarufu wa mavazi,Mustafa Hassanali wamejitosa kudhamini shindano hilo .
Awali shindano hilo lilipangwa kufanyika juni 8 kabla ya kusogezwa mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya warembo kuwa katika mitihani pamoja na mafunzo yao kwa vitendo ‘Field’.
Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alimesema kwamba Shear lenye matawi yake jengo la Millennium Tower na Mlimani City linajihusha na uuzaji wa vipodozi halisi ‘original’ kutoka nje ya nchi litatoa vipodozi kwa warembo watakaoshiriki,huku Hassanali atatoa zawadi ya magauni ya warembo.
Alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea ambapo leo warembo hao ambao awali walikuwa wakifanya mazoezi kwenye hoteli ya Lamada, jana walihamishia kambi yao kwenye hoteli ya Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Dina ameongeza kuwa mpaka sasa wameshapatikana warembo 13 ambao wapo chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na dansa aliyepata kufanya vema miaka ya nyuma, Bob Rich.
“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.

No comments:

Post a Comment