Saturday, 17 November 2012

BALALI YUPO HAI ON TWITTER!

Wote tunafahamu kuwa aliyekuwa gavana wa benki kuu ya Tanzania Daudi Balali alifariki dunia tarehe 16.05.2008 huko Boston, Marekani na kuzikwa huko huko.


Lakini kwa watumiaji wa Twitter watakuwa wanamfahamu Daudi Balali wa kwenye mtandao huo ambaye ameendelea kumuumiza vichwa vya watu wengi kuwa ni nani huyu aliye nyuma ya akaunti hiyo na akiendelea kudai kuwa bado yupo hai?October 1 alitweet, 


“Nitakutana na Rais Kikwete na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani."

Anavyoonekana ni msomi haswaa na anaishi nje ya nchi. Ni mtu makini, ana hoja, anaijua siasa ya Tanzania na yupo consistent! Hivi karibuni mtu huyo alidai kuwa amekuja Tanzania na kulala kwenye hoteli iliyo karibu na ofisi yake ya zamani.


“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” alitweet November 13.


Kutokana na kile anachokiandika anaonekana kuwa ni kada mzuri wa CCM na leo ameibuka na kutabiri anguko la CHADEMA kwa kutweet,“Chadema will die by disintegration. Zitto Kabwe and 3 other prominent members will move to CCM,the rest will form 2 new political parties."


Anasema CHADEMA itavunjika ambapo Zitto Kabwe na wanachama wengine watatu wa chama hicho watahamia CCM na wengi wataanzisha vyama viwili vipya vya siasa.

Hata hivyo anadai ameamua kuondoka nchini mapema na kurudi Gaithersburg, Maryland kutokana kuhofia usalama wake.


“I am leaving Dar es Salaam tonight instead of Wednesday on security reasons.”


Mwisho ameendelea kusisitiza kuwa kweli yupo hai kwa kutweet:


I AM REAL. TAKE IT OR LEAVE IT. TWITTER IS THE MESSENGER. THE SURPRISE IS YET TO COME.
http://freebongo.blogspot.com/2012/11/maajabudaudi-balali-aibuka-na-kudai.html

No comments:

Post a Comment