Friday, 9 November 2012

MAREHEMU FRANCO MAKIADI ULIKUA WAPI MIAKA HII YA 80??NAKUMBUKA SIKU KAMA HIZI ZA WEEK-END MIAKA HIYO MDINGI ALIKUA AKIRUDI NYUMBANI MIDA YA JIONI TOKA MIHANGAIKONI.
MKONONI AKIWA NA SAFARI LAGER ZAKE ZA KUTOSHA,NA MARA NYINGI AKIFIKA NYUMBANI BAADA YA KUPUMZIKA KIDOGO BASI ILIKUA NI LAZIMA AKAE PALE SEBULENI KWENYE MUSIC PLAYER YAKE KWENYE KONA PEMBENI.

MDA HUO SISI TULIKUA TUNAZUGA TUNA BIDII KWELI YA KUSOMA HAPO SIKU HIYO ANATUKUTA TUKO CHINI KWENYE SIMENT(ENZI HIZO UKIWA NA KAPETI WE BILL GATE)NA MADAFTARI TUNAZUGA KUJISOMEA(WALAH ILIKUA KAMBA TU).
BASI YULE MSHUA AKIRUDI SIKU HIZO NAKUMBUKAALIKUA AKIWEKA SANTURI ZA FRANCO(HASA HIYO PICHANI JUU) ZILIKUA ZA KUTOSHA KWENYE MAKTABA YAKE,ZINGINE KAMA  ZA SAM MANGWANA,ORCHESTRA VEVE,VIVA LA MUZIKA NA TABU LEY PIA ZILIKUWEPO,LAKINI ZA FRANCO NDIO ZILISHIKA MPINI.

MDINGI HAPO ALIKUA ANAFUNGUA SAFARI YAKE(SIO MBUYU,ILE REAL) MOJA BAADA YA NYINGINE,KUSEMA UKWELI ILE SAFARI YA ZAMANI ILIKUA INA KAHARUFU KATAMU SANA,BASI MI NILIKUA NAMPIGA CHABO LA KISHKAJI HUKU (NIKITAMANI KALE KAHARUFU(KAHARUFU TU KA BIA JAMENI).

NA MSHUA BAHATI NZURI ALINISHTUKIA KWA HIYO KUNIJALI SANA SANA ALINIACHIA KIZIBO CHA BIERE ANGALAU NIMALIZANE NACHO,NA MIMI SIKUWA NAJIVUNGA NILIKUA NAPOKEA NAKINUSA HICHO KIZIBO,NA KINGINE NA KINGINE MPAKA MSHUA AMALIZE VYUPA VYAKE VYOTE AAH NAMIE NIMALIZIE KUNUSA VIZIBO VYOTE NAKUA NIMEBEMBEA NAKASTIMU KIAINA.
BAADA YA HAPO ILIKUA NATAMBAA TARTIIBU MPAKA KWENYE KITANDA CHANGU CHA SPRING NAANGUSHA MBONJI HUKU NIKIOTA NDOTO KIBAO ZA KUWA MKUBWA ILI NA MIMI NIZITANDIKE BILA MIKWARUZO HUKU WANANGU WAKINIDEKU.

KASHESHE ILIYOPO SASA NDIO HII,HIVYO NDO NISHAKUA BABA MWA-FULANI FULANI(KIVINGINE NISHAKUZWA).

VIJANA NDO HAO WANAREFUKA,AFADHALI YULE WA NYUMBANI KULE TUTAELEWANA(YE HUWA ANAULIZA TU HIVI BABA UNAPENDEA NINI HII?)NAMIE NAMWAMBIA KUA UYAONE,NA HACHELEWI KUULIZA NIIONE BIA?SI HII HAPA NAIONA.
HUYU BWA-MKUBWA MWINGINE HAPA NAONA ANA-ADOPT TABIA ZA KINA MR ANDASH LUNDQVIST NILSON,(NIMPE KIZIBO KWELI CHA NORLAND GULD ANUSE???)TAFADHALI BANA(SIJIPENDI?).

SASA NAONA KABISA NDOTO ZANGU ZILE ZA KUPAKAZA KIBABA-BABA AFRICA KAMA MSHUA ZINAYAYUKA HIVI HIVI MWEEEH!

WEEK-END NJEMA WADAU

No comments:

Post a Comment