Saturday, 17 November 2012

DIAMOND AKACHA KUMVISHA PETE NAJMA KWENYE BIRTHDAY YAKE

STAA wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond akiwa katika pozi

 Najma kushoto akiwa na dada yake anayefahamika kwa jina la Lady Na
 
Keki iliyo andaliwa kwa bethdei hiyo

STAA wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati aliikacha sherehe ya kuzaliwa ‘bethdei’ ya demu anayedaiwa kutoka naye kimapenzi kwa sasa, Najma, Risasi Jumamosi lina mkasa mzima.

Sherehe hiyo ilifanyika Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwa dada wa Najma (jina halikupatikana mara moja) aishiye Mbezi ya Afrikana, Dar.
Baadhi ya waalikwa walikuwa wakihoji alipo Diamond kwa vile mchana kutwa wa siku hiyo mitandao ya…
Stori:Musa Mateja
STAA wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati aliikacha sherehe ya kuzaliwa ‘bethdei’ ya demu anayedaiwa kutoka naye kimapenzi kwa sasa, Najma, Risasi Jumamosi lina mkasa mzima.
Sherehe hiyo ilifanyika Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwa dada wa Najma (jina halikupatikana mara moja) aishiye Mbezi ya Afrikana, Dar.

Baadhi ya waalikwa walikuwa wakihoji alipo Diamond kwa vile mchana kutwa wa siku hiyo mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari vya kielektroniki viliripoti kwamba Diamond ataitumia bethdei hiyo kumvisha pete ya uchumba Najma.
Mpaka inatimia saa 6:30 usiku, Diamond alikuwa hajatokea na baadhi ya waalikwa, akiwemo dada wa Diamond na wacheza shoo wake waliamua kutimka kwenye eneo la tukio.
Katika kuondoa machungu ya ‘kutelekezwa’ na sherehe yake, habari zinadai, Najma na dada yake waliamua kuibeba keki ya shughuli kutoka Mbezi  hadi Ukumbi wa New Maisha Club, Masaki, Dar ambapo pia kulikuwa na sherehe kama hiyo ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz.

Akizungumza na paparazi wetu siku iliyofuata,  Diamond alijitetea kuwa hakuweza kuhudhuria kwenye sherehe ya Najma kutokana na kutingwa na shughuli za uandaaji wa video ya wimbo wake mpya wa Nataka Kulewa.
“Nilishindwa kwenda kwenye bethdei ya Najma kwa sababu nilikuwa na kazi nyingi za kuhakikisha video ya wimbo wangu mpya inakamilika siku mbili hizi,” alisema Diamond.

GPL

No comments:

Post a Comment