Friday 16 November 2012

UWEKEZAJI KATIKA ENEO LA POLISI OYSTERBAY, MANISPAA YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM



·        Eneo la Polisi Oysterbay halijauzwa na haliuzwi.
·        Eneo linalohusika sio Bwalo la Polisi bali Polisi Oysterbay.

·        Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetafuta mwekezaji kwa lengo la kuwekeza katika eneo la Polisi Oysterbay lenye ukubwa wa ekari  24. Uwekezaji huo utawezesha kujengwa kwa nyumba za makazi 350 ya Polisi katika maeneo ya Mikocheni na Kunduchi jijini Dar es Salaam na Kituo cha Polisi cha kisasa katika eneo hilo la Oysterbay.
·        Mshauri Mwelekezi wa Mradi huo ni Bureau for Industrial Cooperation (BICO) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
·        Mwekezaji aliyepatikana baada ya kufuata taratibu zote za Manunuzi ya Serikali kufanyika ni Mara Group Ltd. ya nchini Uganda.
·        Tenda ilitangazwa kimataifa.
·        Kampuni 10 zilishiriki katika tenda hiyo.
·        Mkataba wa Awali kati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwekezaji huyo umesainiwa tarehe 23 Juni, 2012.
·        Gharama za uwekezaji katika eneo hilo ni karibu shilingi 426.6 bilioni.
·        Kufuatana na Mkataba wa Awali, Mwekezaji huyo atajenga nyumba za makazi 350 kwa ajili ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam na Kituo kipya cha kisasa cha Polisi katika eneo hilo, kwa gharama ya shilingi 31.6 bilioni.  Fedha hizi zitalipwa kutokana na tozo atakalokuwa analipa Mwekezaji.
·        Kufuatana na Mkataba wa Awali, Mwekezaji atalipa tozo la shilingi 4.36 bilioni kila mwaka kama malipo ya matumizi ya ardhi na majengo na tozo hili litakuwa linapanda kufuatana na mwenendo wa uchumi wa nchi.
·        Kufuatana na Mkataba, ardhi na majengo yote atakayojenga Mwekezaji yatabaki kuwa ni mali ya Serikali na  yeye atakuwa mpangaji tu.
·        Mwekezaji atajenga Maduka makubwa (Shopping Malls), Hospitali kubwa ya kisasa, Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya kisasa, Ofisi za kukodisha, Makazi ya kukodisha na Maeneo ya maegesho ya magari.
·        Mradi utanarajiwa kuanza mwezi Julai, 2013 baada ya kusaini Mkataba.
·        Mkataba wa Mradi ni wa miaka 50.
(Unaweza pia kutembelea Tovuti ya Wizara, www.moha.go.tz kupata taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari tarehe 14 Novemba, 2012).

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment