Wednesday, 28 November 2012

MAZISHI YA SHAROMILIONEA KATIKA PICHA


Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea enzi za uhai wake.
Waumini wa Kiislam wakiwa katika Ibada ya Kuuswalia Mwili wa Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea aliefariki kwa ajali ya Gari hivi karibuni huko Muheza,Mkoani Tanga.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea likiwasili Nyumbani tayari kwa Taratibu za Mazishi yaliyofanyika leo kwenye Kijiji cha Lusanga,Wilayani Muheza,Mkoani Tanga.
udogo ukitupiwa kaburini wakati wa mazishi ya Msanii wa Muziki na Filamu hapa nchini,Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea,ambayo yalihudhuliwa na Watu mbali mbali hapa nchini,wakiwemo viongozi katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.
Muigizaji Maarufu hapa nchini,Mzee Athuman Amri a.k.a King Majuto ambaye ni Baba Mdogo wa Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea akitupa mchanga kaburini wakati wa Mazishi ya Sharo yaliyofanyika leo katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.
 
 kuna waliopoteza fahamu

 Nape Nnauye alikuwepo pia kutoa pole za chama

Mwana FA KITOA POLE KWA NIABA YA WANA BONGO FULEVA


WASANII MBALIMBALI WALIFIKA KUMUAGA MAREHEMU
Vijana wakiwa wamepanda mnazi kuona mazishi ya Msanii wa Muziki hapa nchini,Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.Picha na Bashir Nkoromo.

No comments:

Post a Comment