Saturday, 17 November 2012

unazikumbuka enzi hizi mdau??enzi hizi sasa sikuwa mzee wa mabolingo kama hivi sasa(unajua uzee tena)kwa kumbukumbu yangu kwanza nyimbo ya kwanza(ride on time-black box) nakumbuka miaka hiyo familia ilikua inaishi mbeya,ila kuna mdogo wangu aliyenifuata Imma yeye alikua anaishi Dom,tena pale iringa road jirani na shillam disco na disco toto alikua hakosi,basi ikawa tena ndo katuzidi ujanja.

nakumbuka alipokua akija Mbeya miaka hiyo mdingi alikua anatuonea sana kwa maneno,dogo alikua akiwekewa hasa hiyo nyimbo ya kwanza hapo alikua anaruka breka pale sebuleni hapatoshi,sie tunabaki tumekodoa mijicho tu.mdingi hapo si kujisifia huko kwamba pale ndio amezalisha sio sie maboga tu(aah namie nilikua namuwekea dogo akiba yake ya makwenzi baadae)si unajua jealous tena ya kuchukua ujiko.

badae baada ya mdingi kututoka nasisi tukatimka Mbeya na break ya kwanza ilikua Dom,pale nikakutana na dogo ndio namimi nikazijua safari za kwenda disco toto zikaanza(Mbeya ilikua haiwezekani,dingi atanyonga mtu)
hapo namm kidogo ushamba wa mbeya ukaanza kunitoka,mdogo wangu yule alikua chakaramu kweli maana mama yake aliyekuwa anakaa naye alimpa freedom ya kujiachia(si sana)

baadae nakumbuka kuanza kujua utamu wa disco(sio toto tena)ilikua mitaa ya Singida.miaka hii nakumbuka TUKICHEZA disco people`s clup na DJ alikua mtoto mmoja wa Adam MWAKANJUKI akiitwa Aliko.baadae ndio lilifunguliwa disco tena matata sana pale town nyuma ya stand(matata wapi ilikua kama nyumba ya mtu ya kukaa tu)

katika hilo disco ilitokea kukutana vichwa kama kuna dogo mmoja tulikua tunamuita bahati msomali alikua anacheza sana hizi nyimbo,kuna yule mcheza shoo wa stono muzika(loving chitoto nae tulikua nae pale ye akijiita lady madona na nyimbo hizo ulikua humuachi.

mi nilikuwemo lakini sababu ya ushindani kuwa mkali nikahamia kwenye bolingo hasa za Aurlus mabelle huku rafiki yangu nabil akiwa mkali za Bileku Mpasi.

kwenye disco hilo kulikua na Dj mmoja anaitwa Pailonga,wenye disco walimleta toka dar miaka hiyo na alikuja na kaseti zina vyombo vya kutosha.ALIKUA anatuchezesha disco balaa na alijua kuzipanga nyimbo.

ila kama unavyojua tena Singida wababe kibao disco likiisha lazima mbaki humo maana nje huko mapanga yalikua yanatembezwa kama buchani,mademu wanabebwa live band.

baadae ikaja funguliwa Singida Motel,akaja Black Moses,Diga diga,Kelly John na dada mmoja mkali akijiita Queen Farida(alikuja ugua uchizi mnyamala pale akafa)na Flora"TINGISHA" A.K.A lango la jiji.walipiga show pale singida nzima ikatikisika.

baadae kule yakafunguliwa madisco kadhaa ya kisasa hasa Salma Discotheque.
waliopo Singida watatueleza kilichoendelea maana mi nilisepa mitaa hiyo kipindi hicho nikawaachia mji wao wenyewe.

NGOJA NIWAHI BOX WADAU TUTAENDELEZA HII SIKU INGINE,AU KAMA UNA STORO YAKO TUPIA COMMENT HAPA TUIWEKE HEWANI.

No comments:

Post a Comment