Friday 27 May 2011

Babu ataka vizuizi, ushuru vipunguzwe


 Send to a friend
Thursday, 26 May 2011 22:39
MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila, ameiomba serikali kupunguza vizuizi vya barabarani na  vituo vya kudai ushuru kwa magari yanayopeleka wagonjwa Samunge kwani vimekuwa kero kwa wagonjwa.

Mchungaji Mwasapila aliliambia gazeti hili jana kuwa baadhi ya vizuizi vya barabara na vituo vya ushuru wa magari hayo vimegeuka vitegauchumi vya baadhi ya watu

"Wagonjwa na madereva wanalalamika kunyanyaswa katika vizuizi kwa kudaiwa fedha bila sababu na pia kuwapo mlolongo wa ushuru barabarani, hasa kwa magari toka nje ya nchi, nadhani sio haki,"alisema Mwasapila.

 Alisema kwa sasa kutoka mpakani mwa Tanzania na Kenya na kutoka wilayani Bunda hadi Samunge kuna vizuizi vya barabara zaidi ya saba na vituo zaidi ya vitatu vya ushuru.Katika hatua nyingine, raia wa Uingereza na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakiwamo maofisa wa jeshi, jana walitua Samunge na kupata tiba.

Raia hao wa kigeni, walitua Samunge kwa helikopta mbili za kukodi wakitokea uwanja wa ndege wa Arusha
Waingereza waliotua Samunge wanatoka katika Mji wa London, ambao ni Manoj Jethwa, Keval Jethwa, Dharika Jethwa na Nita Jethwa.

Wakongo waliojitambulisha walikuwa ni Mbuyi Meda, Nyago Mulonda na  Foola la Eutche ambao katika kundi hili mmoja aliyetajwa ni brigedia katika jeshi la Kongo.Pia, jana kulikuwa na raia 250 kutoka nchini Kenya ambao walifika kijijini hapo na kupata tiba kisha kuondoka muda mfupi baadaye.

mwananchi

No comments:

Post a Comment