Thursday 5 May 2011

WEMA SEPETU ATINGA MAHAKAMANI KUSOMEWA SHITAKA LA UTOVU WA ADABU

 
 
 
 
 
Aliyekuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu (27) , mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la kutukana hadharani.


Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alimtukana matusi ya nguoni msanii wa kizazi kipya, Raheem Rummy 'Rais wa masharobaro' ambapo mshitakikosa lake.


Hata hivyo mshitakiwa huyo alidai mahakamani hapo kuwa aliamua kumtukana mshitakiwa kwa sababu ya dharau zake alizokuwa anamfanyia.


''Mheshimiwa Hakimu si kawaida yangu kutukana ovyo ovyo, lakini hasira zimenifanya nifanye hivyo na ndiyo maana nimekubali kosa langu.


Mbele ya Hakimu Mariamu Masamalo, ilidaiwa na Karani Sharifa Dunia kuwa, Aprili 11 mwaka huu Kinondoni, mshitakiwa alimtukana mlalamikaji huyo na kesi imehairishwa mpaka Aprili 18 mwaka huu.


2 comments:

  1. Hivi Mdada huyu Mrembo si ndiye aliwahi kushtakiwa tena na Yule muzee wa Mabongo Muvi KANUMBA kwa fujo hadharani?

    Mdada Mrembo lakini! Ila ndio hivyo hata kama anatabia nzuri ikiwa inarudiarudia hadharani watu wataanza kuona kiunganishi cha fujo hadharani ni yeye!

    Ni wazo tu ingawa nahisi ningekuwa namfahamu ningemkumbusha kuwa yeye ni maarufu kwa hiyo akumbuke hilo pia kuwa anaonekana na kukumbukwa kirahisi zaidi hata akikojoa pembeni ya barabara kuliko siye wengine!


    Na namtakia kila la kheri!

    ReplyDelete
  2. ndio yeye mkuu nadhani hajielewi tu,wengi tunataka kumpa ushauri lakini naona kashindikana.ni kumuacha tu muda utampa lesson nzuri sana.

    ReplyDelete