Saturday 14 May 2011

HASHEE THABEET ARUDI BONGO KIMYA KIMYA



Staa anayeiwakilisha vyema Tanzania kupitia mchezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Hasheem Thabeet (pichani) ‘ametimba’ Bongo kimya kimya na kusababisha watu kumshangaa kwani siyo kawaida yake.

Thabeet anayepiga mzigo kwenye Timu ya Houston Rockets inayoshiriki ligi ndogo ya NBA, juzikati alitinga ndani ya Ukumbi wa Bilicanas mishale ya saa 6 usiku akiwa na washikaji zake wanaodaiwa kutoka nao pande za kwa Obama.

“Siamini kama huyu jamaa ni Hasheem, tumezoea kila anapokuja nchini lazima tuwe na taarifa za ujio wake, lakini kitendo cha kuja ghafla kinatupa maswali mengi kama kweli bado anacheza katika timu hiyo au amefukuzwa,” alisema mmoja wa wadau waliokuwa ndani ya ukumbi huo aliyejitambulisha kwa jina la Doto.

Alipoulizwa juu ya uamuzi wake wa kuingia nchini kimya kimya, Hasheem ambaye ni mchezaji bora wa mwaka 2010 nchini Tanzania alisema kuwa, amerudi kwa ajili ya mapumziko mafupi na kuja kuwasalimia wazazi wake.

Kama hakutakuwa na mabadiliko ya ratiba yake, staa huyo aliyewahi kupiga mzigo na Memphis Grizzlies atakaa Bongo kwa takribani wiki tatu.

GPL

2 comments: