Wednesday 11 May 2011

BARUA YA WAZI KWA WEMA SEPETU TOKA KWA MDAU





Kwako,
Mpendwa dada Wema Sepetu. Naamini u mzima kiafya na unaendelea vizuri na mchakato wa kutafuta mkate wa kila siku.
Kwanza kabisa, pole kwa matatizo. Nilisikia kuwa juzi ulipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumtolea maneno makali Bob Junior. Yataisha tu...usijali.

Nimeona leo nikuandikie barua dada yangu, maana nahisi kama hufahamu kinachoendelea huku uswahili. Washkaji wa vijiweni  wamebadilisha stori, wanakuzungumzia wewe. Siyo Barcelona wala Arsenal tena, ni wewe tu. Unajua wanajadili nini kuhusu huyo Wema?

Ngoja nikuambie...wanazungumza kuhusu haya matatizo yasiyoisha unapokuwa katika ‘relationship’. Tatizo ni nini? Hivi, unakumbuka kipindi kile ulipotwaa taji ya Miss Tanzania? Wiki chache tu, yakaibuka mambo...kwamba ulikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasanii wawili wa Bongo Fleva (kwa nyakati tofauti), ingawa mpaka leo unaendelea kukanusha.

Hayo tuyaache, hebu tuanzie pale ulipokuwa na Kanumba (Steven), baadaye ukahamisha majeshi kwa mjasiriamali Jumbe Yusuf Jumbe.
Nini kilitokea? Pamoja na kwamba ulikuwa umeachana na Kanumba, maneno yakaanza kiasi cha kuvunja vioo vya gari lake, mwisho wake ukawa Segerea! Aibu kiasi gani? Niliamini tukio lile lilikupa funzo lakini kumbe...!

Sitaki kufuatilia sana mambo yako ya ndani, lakini nakumbuka baadaye ulikuwa katika himaya ya mwanamuziki wa Twanga Pepeta Chalz Baba. Mkavuma kweli kweli. Kila mahali mlikuwa pamoja huku mkijinadi kwenye vyombo vya habari kwamba mngefunga ndoa. Uhusiano wenu ukawa gumzo jijini, lakini baadaye ukasafiri kwenda Marekani.

Ukiwa huko, uhusiano ukaanza kuyumba, uliporudi Bongo, ukaangukia kwa Diamond. Mapenzi yamekuwa ‘hot’ ile mbaya ingawa hivi sasa inaelezwa kwamba kuna harufu ya kuvurugika!

Lakini ukiwa na Diamond, ukakumbwa na hili balaa linalosumbua sasa hivi...kesi na Bob Junior ambaye ana bifu na boyfriend wako Diamond. Sitaki kuingilia sana suala hili, maana lipo mahakamani, lakini cha kujiuliza hapa, kwanini haya yote yanatokea?

Wema, nadhani kuna maeneo unatakiwa kujikagua. Kuna mahali kuna tatizo. Mosi, kujitambua na kuthamini thamani yako kama msichana uliyepata bahati ya kushika wadhifa mkubwa wa Miss Tanzania 2006. Hiyo ni heshima ambayo haiwezi kufutika. Ukisimama sehemu yoyote utajulikana kama Miss Tanzania.

Ni hadhi hiyo Wema. Hadhi ambayo inahitaji kutendewa haki. Naamini ukitulia na kujichunguza utagundua ni wapi unaposea. Nitakupa mwanga wa mahali pa kuanzia.
Kwanza; chunguza marafiki zako, maana kama ukiwa na marafiki wenye ushawishi wa kufanya mambo mabaya, utajikuta na wewe unafanya vitu kinyume na jamii halafu mwisho wa siku, unabaki na aibu zako mwenyewe.

Pili, nakushauri kabla ya kuingia kwenye uhusiano ni vizuri kumchunguza na kumjua vizuri huyo mtu ambaye unataka awe mpenzi wako.
Unaweza kuwa na mpenzi mwenye tabia za hovyo na ushawishi hasi, ambao utakufanya na wewe uwe mfuasi wa tabia zake, mwisho wake unaishia pabaya. Jichunguze, wapi unapokosea? Kujua tatizo ndiyo mwanzo wa kusonga mbele katika kufanya mabadiliko.

Naamini ukisoma maandishi ya barua hii kama simulizi za kusisimua, hakuna utakachoelewa, lakini ukisoma kama waraka kutoka kwa mtu ambaye anapenda mafanikio yako, utabadilika na kuwa bora zaidi. Wewe ni staa Wema. Hebu ishi kistaa.
Ahsante kwa kusoma barua yangu.
Wako katika kuwekana sawa,


NENO LANGU
KUNA KA UKWELI HAPO LAKINI JE WEMA ATAUCHUKULIA VIPI HUU USHAURI?TATIZO WATU HAWAJAJUA KAMA WEMA ANA KAUGONJWA KANAITWA "PENDAPENDA" SIKU KAKIISHA ATAACHA TU BANDIKA BANDUA.

DALILI ZA MGONJWA WA PENDAPENDA

1.KUWEWESEKA KILA MARA ANAPOMUONA KIJANA MTANASHATI MBELE YAKE
2.KUPATWA NA JOTO NA KUONA VIMULIMULI VYA KITANDA KILA AKIMUONA H.B.
3.KUMSAHAU MPENZI WAKE KILA AKIMUONA H.B MPYA
4.WIVU KUPINDUKIA NA KUWA NA UGOMVI WA MAWE
5.KUPOROMOSHA MITUSI KILA AKIONA ANAARIBIWA TIMING
6.
7.
8.
9.
10.

TO BE CONTINUED

MWINGINE ANAYEJUA DALILI ZA UGONJWA PENDA PENDA TUSAIDIANE WADAU NIMESAHAU

No comments:

Post a Comment