Thursday 5 May 2011

BANZA STONE AJIUNGA NA EXTRA BONGO

BANZA STONE NA ALLY CHOKI

Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo Kamalade Ally Choki amesema, tayari wamemchukua mwanamuziki machachari na mtunzi mahili Ramadhan Masanja, au Banza Stone kama wanavyomuita mashabiki wake.

Ali Choki ameyasema hayo wakati alipoongea leo mchana kwa njia ya simu, akiwa pamoja na mwanamuziki Banza Stone jijini Dar es salaam, Choki amesema kwamba kutokana na uwezo wa Banza Bendi ya Extra Bongo imeona ni muhimu kumuongeza kwenye safu ya uimbaji na utunzi, pia mwanamuziki huyo mwenye uwezo mkubwa wa kutunga nyimbo.Naye Banza Stone ameithibitishia FullShangweBlog kwamba tayari kila kitu kiko sawa, na yeye ataanza kuonyesha makeke yake katika ukumbi wa Mzalendo Pubu kesho, wakati bendi hiyo itakapofanya onyesho lake kwenye ukumbi huo, uliopo jengo la  Milenium Makumbusho jijini Dar es salaam.

Ameongeza kwamba siku ya ijumaa atafanya mambo pamoja na Extra Bongo kwenye ukumbi wa Meeda aliopo Sinza jijini Dar es salaam, na kwa sasa anatengeneza nyimbo kali kwa ajili ya kuzitambulisha kwa mara ya kwanza katika bendi hiyo
 
 
 chanzo:FullShangweBlog
 
MY WORDS
 
AFADHALI CHOKI UMEMKUMBUKA HUYU JAMAA YAKO BANZA,KWA TUNAOWAFAHAMU MLIKOTOKA TUNASIKIA FURAHA SANA MMEJIUNGA TENA,SASA NI MUDA WA KUPIGA KAZI INAVYOTAKIWA NA TUNATUMAINI KWAMBA BANZA CHINI YAKO CHOKI HESHIMA ITAKUWEPO.

No comments:

Post a Comment