Sunday 8 May 2011

VIJIMAMBO VYA WEMA SEPETU



Habari zilizotua katika dawati la gazeti hili zinadai kuwa, wasanii maarufu Bongo waliokuwa wameangukia kwenye dimbwi la mapenzi, Wema Abraham Sepetu na Naseeb Abdul ‘Diamond’, wamemwagana.

Chanzo chetu cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, uhusiano wa wawili hao umefikia kikomo baada ya siku chache zilizopita kila mmoja kuonekana kutokuwa na ‘taimu’ na mwenzake.

Ikadaiwa kuwa, wa kwanza kumpotezea mwenzake ni Diamond ambaye amekuwa haoneshi ushirikiano kwa mwenzake hasa katika matatizo ya kesi inayomkabili ya kumtusi msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Raheem Nanji ‘Bob Junior’.
“Penzi la Wema na Diamond imebaki stori, sasa kila mmoja anaonekana kuwa na maisha yake, labda wakae chini na kumaliza tofauti zao kisha kurudiana tena lakini kwa jinsi ninavyoona mh! Sijui…,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:

“Kama ulikuwa unawafuatilia sana utakuwa umegundua kuwa hawana mbwembwe kama ilivyokuwa awali. Wema anaenda klabu peke yake na hata alipopelekwa polisi na Bob Junior, Diamond hakwenda kumwekea dhamana badala yake alienda mtu baki.”
Aidha, katika kudhihirisha kwamba uhusiano wa mastaa hao umeyeyuka, hata Wema alipapondishwa kizimbani juzi (Jumatano) kujibu shitaka la kumtusi Bob Junior, Diamond hakuonekana kabisa mahakamani.

Matokeo yake waliokuwa wakihaha kumuwekea dhamana mrembo huyo walikuwa ni marafiki wa Wema ambao ni Jacqueline Pentzel na Rose Ndauka, mazingira yaliyoashiria wazi kwamba, penzi la mastaa hao limeingia mdudu.
Wenyewe wanasemaje?

Kufuatia taarifa hizo, gazeti hili lilifanya jitihada za kuzungumza na wahusika ambapo Diamond kwa upande wake hakuwa muwazi kuanika ukweli licha ya maelezo yake kuonesha dalili kuwa hayuko tena na Wema.

“Niko studio na kuhusu habari hizo kwa sasa sina la kusema ila nina mengi ambayo nitayaeleza hivi karibuni, niko bize sana nitakutafuta lakini ifike wakati kila mtu abebe mzigo wake,” alisema Diamond.
Naye Wema alikiri kutofautiana na Diamond lakini mwenyewe akabaki na imani kwamba, watakaa na kuyamaliza.

 “Jamani kwa sasa sihitaji kuongea na waandishi wa habari, maana mambo ni mengi mno. Katika haya yanayotokea Diamond alikaa pembeni ili asionekane yuko karibu sana na mimi, japo kuna tofauti baina yetu lakini naamini tutayamaliza,” alisema Wema.

chanzo.global publishers

No comments:

Post a Comment