Tuesday 17 May 2011

MSAFIR DIOUF AANZA KAZI TENA


baada ya kukutwa kaunyaka mtindi inavyopaswa na kuutandika usingizi wa pono nyuma ya stage ilibidi uongozi wa twanga umpe kalikizo kidogo ili ajitambue maana.....
sasa huyu bwana karuhusiwa tena kuendelea kuwatumbuiza mashabiki.tatizo la diouf hajui kwamba kipaji alichonacho ni adimu sana,twanga wanajitahidi sana kum-maintain lakini jamaa yangu ndo hivyo tena sikio lakufa.
hawa washkaji wawili huyu na banza sijui walilishwa nini,maana ni moja kati ya wanamuziki ninaowafagilia sana bongo lakini tatizo lao ubwii mwingi.wote tunapakaza lakini ikifikia mahali unapakaza mpaka unaangusha gari kama hivi au unajikojolea jukwaani hiyo noma sasa.pakaza kiaina bakisha balance ya kupiga kazi au angalau ya kuunga safari ya kwenda home.
meneja wa bendi bwana martin sospeter amethibitisha kwamba jamaa anatakiwa aripoti leo kazini bila kukosa.
haya mr diouf chance nyingine ndio hiyoo tena una bahati we jembe pale twanga vinginevyo ungekuwa mtaani.



No comments:

Post a Comment