Friday 6 May 2011

MSANII LULU ACHARANGWA VIWEMBE

LIZ-LULU

 Mhusika katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, kwa mara nyingine ametengeneza kichwa cha habari ya kuhuzunisha baada ya kucharangwa viwembe usoni na wanawake wa mjini.

Lulu aliyetimiza miaka 18 hivi karibuni, amefanyiwa unyama huo chanzo kikidaiwa kuwa alifumwa katika pozi tata na mume wa mmoja wa wanawake hao.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha The Number One Bongo Celebritie’s Paper, Ijumaa, Lulu alikutwa na balaa hilo Jumatatu saa 4: 48 usiku ndani ya baa moja (Jina tunalihifadhi) iliyopo Kariakoo, Dar es Salaam.

Baada ya kuinyaka ishu hiyo ikiwa nusunusu, ‘mavuvuzela’ wa Ijumaa walitia maguu katika baa hiyo siku ya Jumanne kwa lengo la kupata mbivu na mbichi za habari kamili ya tukio hilo.

Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa wahudumu wa baa hiyo ambaye hakutaka jina lake lipambe ukurasa huu alisema kuwa, awali mwanaume aliyekutwa na Lulu alizama ‘kiwanjani’ hapo na kupatiwa huduma ‘kama kawa’ kwa kuwa ni mteja wa siku nyingi.

Mhudumu huyo alidai kwamba, haukupita muda mrefu Lulu naye alitimba na kuungana na jamaa huyo kabla ya wanawake hao waliokuwa wametega kwenye gari aina ya Toyota Prado nje kuzama na ‘kumchora’ viwembe usoni.

Alidai kuwa tukio hilo halikuchukua sekunde nyingi kwani wale wanawake walitimka mbio na kuzama kwenye gari lao ambalo lilikuwa ‘stendibai’.
Alimalizia kuwa baada ya tukio hilo watu waliokuwepo waliogopa kutokana na hali ya Lulu aliyekuwa akichuruzika na damu usoni.

Hata hivyo, ilisemekana kwamba walimpatia huduma ya kwanza kwa kumfunga vitambaa kisha jamaa aliyekuwa naye akamuwahisha hospitalini (hakumbuki jina).

Alipotafutwa Lulu kuzungumzia sakata hilo, alitambaa na mistari: “Jamani hali ya uso wangu ni mbaya, si unajua sura yangu ilivyo? Hebu ‘imajini’ ukiiona imechanwa viwembe unapata picha gani? Naona kama ndoto kwani ‘even me, I don’t believe what happened (hata mimi siamini kilichotokea).

“Naweza kumkumbuka mwanamke mmoja, namfahamu kwa jina la Ivon, alinivamia na kuanza kunishambulia huku mkononi akiwa ameshika wembe ambao alinicharanga nao usoni kisha akanisukuma nikadondoka huku nikivujia damu. Shukrani kwa watu walionisaidia.

Lulu aliendelea kudai kuwa, kwa sasa hawezi kuweka hadharani hatua alizochukua ili kutotibua mambo.

“Namshukuru Mungu naendelea vizuri, sitaki mje kunipiga picha, nikiwa kamili nitawaelezea mkasa kamili,” alisema Lulu kisha akakata simu.
CHANZO:GPL

POLE SANA LAKINI USHAKUWA MKUBWA SASA HIVYO KAA TAYARI,MAANA USHAINGIA KWENYE MECHI RASMI NA MADEMU WA MUJINI BONGO WATAKULA SAHANI MOJA NA WEWE.JIANDAE

No comments:

Post a Comment