Tuesday 14 June 2011

AMUUA MKEWE BAAADA YA KUGUNDULIKA MKEWE KAMWAMBUKIZA NGOMA








Rhobi Chacha na Haruni Sanchawa
MWANAUME anayejulikana kwa jina la Lucas John Komba ambaye  amedaiwa kumuua mkewe, Happy Samweli  baada ya kumchoma kisu wakiwa gesti, amefichua siri na kudai amesalitiwa baada ya kupima na kugundua ameathirika na Ukimwi.

Komba aliyezungumza na waandishi wetu akiwa kitandani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikolazwa, alidai siku ya tukio alikumbwa na shetani aliyesababisha amchome kisu mkewe kisha kujitumbua tumbo  kwenye tukio lilitokea Juni 6, mwaka huu.

Tukio hilo lilitokea saa 11. 00  jioni katika nyumba ya wageni iitwayo A Plus Lodge iliyopo  Shekilango Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Wawili hao inadaiwa baada ya kupanga chumba namba 3 walikurupuka wakiwa watupu huku mwanamke utumbo ukining’inia na mwanamume akiwa na kisu tumboni kisha wote kuanguka hatua chache nje ya gesti hiyo.

Lucas  akiwa amelala hospitali hapo alikuwa na haya ya kuelezea kuhusu mkasa huo:
“Mimi sina muda mrefu hapa Dar es Salaam nina miezi miwili toka nitoke Musoma, nafanya kazi ya ulinzi katika Hospitali ya Modern iliyopo Manzese, familia yangu yaani mke na watoto wangu wawili Cristiano (2) pamoja na Stephano (4)niliwaacha Musoma nikawa nawatumia fedha za matumizi kila nipatapo.
“Mke wangu (marehemu)  akanipigia simu na kuniambia kuwa anataka kuja Dar, nikamtumia nauli akafika Juni 18, mwaka huu na tulikuwa tunakaa Mabibo Makutano.

“Alipofika alikuwa anaumwa mara kwa mara, siku moja alizidiwa akalazwa katika Hospitali ya Modern ninayofanyia kazi, Daktari alimpima vipimo vyote ndipo alipogundulika ana ukimwi.

“Tangu alipokuja nilifanya naye mapenzi mara tano ndipo nilipoona ameniharibia dira ya maisha yangu kwani inawezekana ameniambukiza.

“Tuliporudi nyumbani  mke wangu akawa anasisitiza tuendelee kufanya mapenzi kwani kama ni ukimwi tayari wote ni waathirika.

“Kulikuwa hakuna amani ndani ya nyumba. Siku ya tukio mke wangu aliniambia nimpeleke kwa dada yake anayeishi kota za Jeshi  Sinza, tukiwa njiani, tuliona gesti mke wangu akaniambia tuingie ili akanieleze vizuri alikoupata ukimwi.

“Mimi sikubisha tuliingia, akaanza  kunieleza kuwa alipokuwa Musoma alikuwa anaishi na mwanamume ndani ya nyumba niliyomuacha baada ya muda akaja kugundua kuwa ameathirika ndiyo akatakiwa kuja Dar ili anieleze.

Baada ya kunaimbia hivyo, nilimuuliza alikuwa anakosa nini wakati nilipokuja Dar kutafuta maisha nilimuachia biashara ya vyombo na mtaji mkubwa ili aweze kuendesha maisha na fedha nilikuwa namtumia?

“Mke wangu alinituma nikamnunulie maji ya kunywa, niliporudi nikamkuta kavua nguo akitaka penzi akidai sisi sote ni waathirika, nilimpa bila kujua alificha kisu chini ya shuka na ndiye aliyeanza kunichoma.
“Wakati mwenzangu alidhamiria kuniua, mimi nilikuwa na vidonge na sumu ya panya ambavyo nilipanga kunywa ili nijiue kwani niliona kanipotezea dira ya maisha yangu,” alisema Lucas.

Waandishi wetu walipomuuliza kuwa siku hiyo walikuwa wamepanga kwenda kujiua maana kila mmoja inavyoonekana alikuwa amejiandaa,  alisema anajuta kwa kitendo kilichotokea kwani alikuwa ni shetani kampitia.

Alisema alijua mtu akifanya mapenzi na mwenye ukimwi lazima naye aupate, ambapo aliongeza kuwa  anawahurumia zaidi watoto wake ambao wanahitaji matunzo kwa kuwa bado wadogo.

Mwili wa mkewe Happy ulisafirishwa kwenda Musoma kwa mazishi na Lucas habari za kipolisi zinasema Ijumaa iliyopita alisomewa mashitaka ya kuua akiwa hospitalini anakoendelea kutibiwa

source:GPL

INASIKITISHA KWAMBA HAWA JAMAA WALIANZA KUJINYANYAPAA WENYEWE KABLA HAWAJANYANYAPALIWA,ALIYEWAAMBIA KAMA KUWA NA UKIMWI NDIO MWISHO WA MAISHA NANI?
NA PIA MATANGAZO YOOTE YA DAWA YA NGOMA NA ARV,S (USISAHAU KIKOMBE KWA BABU) HAWAJAYASIKIA?
YES INAUMA KUSIKIA MKEO KAPATA NGOMA KWINGINE AKAKULETEA LIVE,LAKINI SWALA KUBWA NI KUSAMEHEANA NA KUENDELEZA MAISHA
SASA WAMECHOMANA VISU MKE KAFA BWANA NDIO HUYO MAJERUHI NA SEGEREA INAMSUBIRI KWA HAMU,
WAATHIRIKA WATOTO NDIO WATAKIONA CHA MOTO KWANI KUANZIA SASA ITABIDI WAISHI KWA KUTEGEA KINA MJOMBA NA MAMA WADOGO.

HADITHI HII INATUFUNDISHA NINI...........?

No comments:

Post a Comment