Friday 10 June 2011

WEMA JELA MIEZI SITA AU FAINI 40,000

WEMA AKIWA NA ALMASI
MISS Tanzania 2006, Wema Sepetu jana alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh 40,000 baada ya kupatikana na hatia ya kumtukana matusi ya nguoni na kumtishia usalama, Raheem Nanji maarufu kwa jina la Bob Junior ‘Rais wa Masharobaro’.

Wema alihukumiwa kifungo hicho na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mariam Masamalo baada ya kuridhishwa na ushahidi wa mlalamikaji uliotolewa mahakamani hapo.

Katika hukumu hiyo, Hakimu Masamalo aliwataka mashahidi hao kutoa ushahidi mbele ya mahakama hiyo, baada ya ushahidi huo hakimu huyo alichukua muda mfupi kupumzika na kutoa hukumu hiyo.

Baada ya hukumu hiyo, ndugu na jamaa wa Wema walijikusanya na kulipa faini ya Sh 40,000 na kuachiwa huru, huku mahakama hiyo ikimuonya mrembo huyo kutorudia kutenda kosa kama hilo. Wema alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 4, 2011.

Aidha, katika tukio lingine Wema alishikiliwa tena mara baada ya kuachiwa huru mahakamani hapo kwa kile kilichodaiwa kutoa lugha ya matusi ya nguoni kwa Rehema Fabian, mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa maelezo zaidi.
chanzo:GPL

No comments:

Post a Comment