Wednesday 8 June 2011

MIKASA YA WEEK END NA MASANGA


pombe bana
sometimes huwa najifikiria kuacha mambo ya kupiga ubwii maana mikasa tunayokumbana nayo si kidogo.
tatizo linakuja kama ukiacha kupata mayi na kukutana na bandugu damu moja kunako nyanja hiyo sijui utafanya nini kingine hasa ukiwa nje ya nchi.
nafikiri utaishia kuangalia TV weee mpaka mwisho TV itakua inakuangalia wewe na  iko siku itakuuliza * wee hutoki?
basi kwenye hivyo vikao vyetu vya ubwii ndipo huwa tunakutana na mikasa yoote ya dunia,na ndio maana unakuta mtu unaweza kunogewa ukashangaa kumekucha kabla hata hujastukia,kisha ukaanza kufikiria tena majibu ya kwenda kujibu kesi nyumbani kwa mama chanja.

huku kwenye ubwii tunakutana na maprofessor wa maproffesoure na saa nyingine huwa hawachelewi kutufungulia darasa bar na kuanza kumwaga lecturer na pwenti za kufa mtu<univesitet of vasagatan>,
sasa ingine utamuona mtu mlevi kumbe anayajua masomo ya kila dizaini ukimuuliza utashangaa ni mjuaji kuliko wanafunzi na ukashindwa kuelewa huyu mlevi kayajulia wapi haya yote?
huwezi kupata jibu mpaka uwe mshirika wa zile sebule zetu za kilaji.
huku tunakutana na watu wa kila aina,saa nyingine huwezi kuamini unakaa na mshirika anakupa store za ajabu mpaka unashangaa.
sebuleni huku tushakutana na watu waliopigania uhuru wa afrika toka mataifa mbali mbali,enzi hizo
waliofanya kazi na idd amini,walioanzisha O.A.U.
kuna kipindi nilishakutana mpaka na waziri mkuu mmoja wa zamani<mkimbizi> wa nchi moja ya kiarabu aliekimbia kwao tukawa tunapiga box wote.
hizo ni baadhi ya faida chache
tukija kwenye hasara hapa ndio point yangu ilipo,kuna tatizo moja la sisi waafrika,mara baada ya kupata pombe au ubwii,huwa tunatafuta ulingo uko wapi tuzichape ngumi.sasa ikifikia hali hiyo ni swala la kuliepuka sana,lakini saa ingine maudhi mengine hayaepukiki.na ndio hapo mtu unaamua potelea karibu unaamua kujibishana ama hata kurudishia pale unapotukanwa au hata kurusha ngumi pale mtu anapokukaba.
kisa cha juzi hapa,baada ya kuombwa na mwadada mmoja nikamrekodie video stejini,kumbuka mziki umechanganya.
namaliza kurudi kurekodi video hiyo nikakae nilipokaa,namkuta bingwa mmoja kakaa pale pale nilipokuwa,na kinywaji yangu niliyoacha mezani anainywa kwa mbwembwe,sasa nikashtuka huyu bwana vipi tena,
lakini sababu jamaa namuheshimu nikaona aah isiwe tabu nikakaa pembeni na kubaki namuangalia tu akiendelea kuteremsha kinywaji yangu kooni kwake kiulainii.
sasa baadae nikaona ni upuuzi kukaa kimya,nikamuuliza
e bana vp naona umekaa nilipokaa na biere yangu utaiteremsha kimikogo kweli.
uliza alinijibuje tena kwa dharau
hawa vijana wanaomba omba bia sana
haya kijana chukua hii,akanipa chupa<kumbuka ni bia zangu hizo> ile ambayo ashapiga mafunda ya kutosha na tena akapiga funda la mwisho kisha eeh chukua ukate kiu kijana.nikabaki namtizama

kisha yule muheshimiwa sana akasema
nawanunulia bia vijana hawa siku zooote hawaridhiki

<sijui kina nani sijawahi kunywa bia hata moja ya huyu muheshimiwa>

pata picha ni hasira kiasi gani ilinipata na baada ya hapo tena sikumbuki niliongea nini ila tu usiku huo haukuisha vyema maana kuna mnunuliwa bia aliyekaa pale aliingilia kati.

anyway unapokuwa kijana saa nyingine ni utumwa,na watu hata ukiwaheshimu vipi saa ingine wanakulazimu uwavunjie heshima,
huo ni mfano tu wa watu wengi wa kila namna tunaokutana nao kila siku kwenye kilaji wanalazimisha kumdharau mtu sababu ni ile ile ya kipuuzi kwamba

<mimi nimekuja siku nyingi hapa vijana mmenikuta hivyo hapa ulaya hamuniambii kitu>

huu ni ushamba wa hali ya juu sana ambao unatakiwa kukemewa kwa namna yoyote,kwasababu badala ya kujitapa kuja siku nyingi ningekuona wa maana sana kama wewe uliyekuja siku nyingi ukanipa mwongozo na mifano hai namna ya kukabiliana na changamoto za hapa ughaibuni.

wazee msituangushe bana,huko sebuleni tunapokutana tupeane ushauri wa mambo ya maana zaidi ya kukimbizana kwa vidosho na kulazimishia umaarufu wa kutoa ofa.


by the way sikukasirika,nilirudi nyumbani na kesho yake nikawa nacheka tu yaliyotokea

No comments:

Post a Comment