Monday 13 June 2011

MAJAMBAZI WAPORA MAMILIONI DAR

Kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni Majambazi wakiwa na Bastora wakitumia usafiri wa pikipiki wamevamia na kupora kiasi cha  fedha kinachokadiriwa kufika tsh 13 milioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam leo asubuhi majira ya saa mbili.
Taarifa zinaeleza kuwa mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya  Full Time Security, Juma Magungu  aliyekuwa analinda katika Idara ya Uhasibu alipigwa risasi na kufa papo hapo
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa gari  lenye namba za usajili SU-36713 aina ya Nisani ikiwa na watumishi Wanne wa Idara ya Uhasibu walivamiwa na kuporwa kiasi hicho cha fedha. Chanzo. (Imeandikwa na Mwandishi wetu kutoka Dar es Salaam
 
CHANZO:MJENGWA BLOG

No comments:

Post a Comment