Friday, 11 May 2012

ANTI LULU:"ATAKAYENIIBIA BWANAANGU NAMROGA"                     Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’.
Na Gladness Mallya

ALIYEWAHI kuwa mtangazaji wa kituo cha televisheni cha C2C cha jijini Dar ambaye kwa sasa anaendesha maisha yake kwa kucheza filamu, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ ametangaza vita kwa mwanaume yeyote atakayemchukulia bwana wake.
Akipiga stori na Ijumaa juzikati, Anti Lulu alisema kuwa kuna mademu anaowajua ambao wamekuwa wakimzengea mchumba wake huyo aliyemtaja kwa jina la Bondi hivyo kueleza kuwa atakayemnasa atamtambua.
“Kwa hili nitamuendea mtu kwa mganga, yaani nitakayebaini anatembea na Bondi nitamgeuza chura.
“Tatizo watu hawajui kuwa nimetoka mbali na mchumba wangu huyo, wanamshobokea kwa lengo la kuniharibia, sasa nitahakikisha napambana na wezi wa penzi langu kwa staili hiyo,” alisema Anti Lulu.

chanzo:GPL

No comments:

Post a Comment