Wednesday 2 May 2012

UTAMU WA NDOA KUSAIDIANA

 

hapo kibongo bongo utaambiwa mume bwege au umelishwa limbwata(kinyama cha kule sehemu)
hapa simsemei mtu yeyote maana kusema ukweli mi mwenyewe nshaosha vyombo ile mbaya nyumbani,wakati mama yuko mguu juu anabadilidha chanel tu sebuleni,kimila za kwetu afrika nadhani  ingekua anafanya hivi  hivi nadhani mpaka sasa meno yake yangekua yanahesabika,lakini ndo hivyo bana tumeamua kukimbilia nchi za wenzetu wenye usawa basi inabidi kukubaliana na hali halisi.
kuna ugumu wake kufanya kazi za nyumbani wakati mke yupo,lakini licha ya ugumu huo inabidi uonyeshe ushirikiano maana ukileta ubishi utajikuta kwa psychtriastic na ukiendeleza ubishi iko siku utakuta talaka ishaandikwa na vinguo vyako vimeshawekwa kwenye viroba vya IKEA vinakusubiri ufike tu upewe,sometyme unaweza kurushiwa hata kutokea balcony
na hapo ndio basi tena utakua tayari una nyongo mbaya na hutatamani tena kuwa na muzungu wife,lakini ukichukulia vitu easy,aaah vyombo unaosha,unafagia nyumba,unampikia mama rojo la maharage na wali ili akimaliza kuangalia tv unamuita aje mezani ale,ikiwezekana baada uya kula muda wa ziada baadae unamfanyia hata scrub ya miguu na kumkata kucha,aah hapo baba utashangaa zawadi kibao mama kila akirudi nyumbani ana kamzigo amekuletea mume.

1 comment:

  1. Ukweli mtupu na si kwa mke mzungu tu hata sie weusi

    ReplyDelete