Thursday 24 May 2012

mbunge wa rombo Mh Joseph Salasini amepata ajali mbaya sasa hivi


 Mbunge Joseph Selasini kapata ajali eneo la Bomang'ombe Mjini, karibu na pale wanapouza nyanya...

Gurudumu moja la mbele la gari alilokuwa akisafiria lilipasuka. Gari likaacha njia likaangukia darajani. Kwa wale wanaofahamu eneo hilo kuna daraja maarufu linaitwa Mjapani.

Alikuwa akitokea Arusha kumtoa baba yake hospitalini. Yeye na Baba yake wamesalimika. Walikuwa wamefunga mikanda. Ndiyo iliyowasaidia. Wengine watatu, mama yake, shangazi yake na mama mmoja mwingine, wamekufa pale pale.

Mbunge anaendelea vizuri. Amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Anaongea.

Tumaini Makene,
Kurugenzi ya Habari - CHADEMA

No comments:

Post a Comment