Thursday, 24 May 2012

SAFARI YANGU MBEYA!


Somewhere near Tukuyu


File:Tukuyu.jpg
 nilipita pia mahali hapa
 na niliikuta hii mashine imepaki inapakia mzigo,nilitamani sana kupiga nayo picha lakini sikuwa na jembe
 
kiwira
wadau wapendwa wa blog hii ya isaackin,msione kulikua kimya hapa nilipata safari kidogo ya kushuka kijijini kupalilia migomba ikiwa ni pamoja na kuji-boost tayari kwa mapambano mengine.
safari yangu ilikua poa nilifika salama na kurudi salama kabisa ingawa magari yanatembea kama ndege barabarani,nimefika nimekula matoki na takapela bila kusahau ngunyani na ugali,na of course jogoo mmoja aliyeshiba alipoteza maisha kwa ajili yangu.nimefurahi kufika huko na kuwaona tena watu wangu wakiwa na nguvu na afya na ilikua raha sana kwakweli,nimerudi salama na nitarejea tena baadaye
nashukuru kwa kuendelea kunitembelea na kuuvumilia kimya changu

No comments:

Post a Comment