Friday 18 May 2012

ATC HEWANI TENA


Kaimu Mkurugenzi wa shirika la ndege la ATC Bw. Paul Chizii kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza mchana huu ambapo wafanyakazi pamoja na watu mbalimbali ambao wamekuwa wakitumia shirika hilo katika kusafiri wameonekana kufurahia sana kuanza kwa safari za shirika hilo

Katika uwanja wa ndege wa Mwanza kutakuwa na hafla fupi ya kupongezana na kukaribisha ndege hiyo ambapo pia keki itakatwa na kuliwa kwa kuashiria uzinduzi rasmi wa safari zake
Abiria mbalimbali wakishuka mara baada ya ndege hiyo kuwasili jijini Mwanza nchana  huu.
Abiria wakishuka kwenye ndege.

 Tayari ndege mpya ya shirika la ndege la ATC aina ya  Boeing 737-500 imeshatua katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro Internationl Airport kwa muda kabla ya kuelekea jijini Mwanza tena na kurudi jijini Dar es salaam katikati aliyeshika ua ni mtangazaji wa Clouds Said Bonge akishoo Love na mashabiki wake pamoja na wafanyakazi wa kiwanja cha ndege cha KIA leo hii katika uzinduzi rasmi wa safari zake.
Hii ndiyo ndege yenyewe ya ATC Boeing 737-500 ikiwa katika kiwanja cha ndege cha KIA muda huu kabla ya kuruka kuelekea jijini Mwanza kabla ya kurejea jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment