Wednesday 12 January 2011

BOBAN APATA NAFASI NYINGINE YA MAJARIBIO SWEDEN



ZALI limeendelea kumuangukia kiungo mchezeshaji, Haruna Moshi ‘Boban’ baada ya kupewa mwaliko mwingine wa kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika timu ya daraja la kwanza nchini Sweden ya Vaspera SK.


Wakati Boban anapewa mwaliko huo, timu ya Sryanska ya Sweden nayo inaendelea kumsubiri arejee nchini humo wiki ijayo baada ya kumrudisha Tanzania na kutaka ajifue zaidi.

Boban ambaye bado ana mkataba na Gefle IF ya Ligi Kuu ya Sweden, yupo nchini akiendelea kujifua ili arejee nchini humo kuendelea na majaribio katika timu ya Sryanska.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, wakala wa kuuza wachezaji anayetambulika na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Damas Ndumbaro alisema tayari wamepokea mwaliko huo ambao umepanua wigo zaidi.

”Kweli tumepata mwaliko na tunaendelea kuufanyia kazi kwa ajili ya kuangalia nini cha kufanya kuhusiana na suala hilo,” alisema Ndumbaro.
Boban alifanikiwa kung’ara akiwa na Gefle IF, hata hivyo alivunja mkataba ghafla na kurejea nyumbani hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa.

Mwaka jana mwishoni Boban alirejea nchini Sweden kwa ajili ya kufanya majaribio na Sryanska lakini ikaonekana hakuwa katika kiwango kizuri, wakaamua kumpa nafasi ya mazoezi zaidi akiwa hapa Tanzania kutokana na kuwa na baridi kali nchini humo.
SOURCE:GPL

KARIBU TENA BANA


No comments:

Post a Comment