Thursday 13 January 2011

P.D.G NDAMA MUTOTO WA NG`OMBE MIKONONI MWA POLISI TENA

P.D.G. NDAMA akigawa wekundu wa msimbazi kwa fally ipupa
wakongo wanajua kuharibu watu,maana wakikuita pedeshee inabidi uzisake kwa nguvu zote ili ulinde heshima(kuwatuza)
nadhani mshawahi kumsikia huyu jamaa,kwanza ni yuleee aliyemuoa mchumba wa NGUZA MBANGU(MIRAESA MBONGO) kama mnakumbuka kipindi mzee nguza viking na wanawe wamepewa ile kesi ya kubaka na kuzawadiwa kifungo.jamaa palepale akamchomekea miraesa na kuoa moja kwa zote ili kumsaidia nguza mbangu kulea.
pili kama mnakumbuka pia jamaa aliwahi kuhusishwa na kesi ya viungo vya albino kipindi cha nyuma.sijui hiyo kesi iliishaje lakini akarudi mtaani,si unajua watoto wa mujini wanajua jinsi ya kucheza na manjagu.safari hii jamaa wamemuotea tena.inadaiwa kuna lori fuso liliibiwa mitaa ya tunduma huko likiwa na mzigo,mafriji,magodoro,na zaga zaga kibao.baada ya hapo jamaa walikimbia na lori hilo hadi bongo kisha wakamuuzia ndama gari na mzigo kwa bei ya mil 4 tu(teh teh)!.nadhani polisi safari hii waliamka maana walipopata taarifa baada ya kufuatilia wakalikuta lori uani kwa jamaa limepaki.na jamaa alipobanwa akawataja waliomuuzia.haya kesi bado iko polisi inafanyiwa uchunguzi(uchunguzi kule maana yake ni kukubaliana atakata ganji bei gani aachiwe)akiweza tutamuona mitaani wakishindwa kuelewana(kama watashindwa) ndio hivyo tena.
habari ya kukutwa na viungo bofya HAPA
habari ya kukamatwa kwa tuhuma za ujambazi bofya HAPA

No comments:

Post a Comment