Tuesday 18 January 2011

MAJADILIANO JUU YA PESA MOJA E.A.C

Sarafu moja Afrika Mashariki yajadiliwa

Mazungumzo yanaendelea Arusha, makao makuu ya Jumuia ya Afrika mashariki nchini Tanzania, juu ya uwezekano wa kuwa na sarafu moja kwa eneo hilo la Afrika.
pesa ya Tanzania
pesa ya Tanzania


Maafisa wanaowakilisha Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, wanakutana kwa siku nne kujadili jinsi sarafu hiyo ya pamoja namna itakavyoafikiwa.
Hii na awamu ya tatu ya kujaribu kuziunganisha nchi za Afrika kwa lengo la kurahisisha na kupunguza gharama za biashara.
Lakini wadadisi wamesema mradi huo utaleta wasiwasi katika eneo hilo kusipozingatiwa kuwepo kwa umoja wa kisisasa kwanza.
BBC SWAHILI.

hayo majadiliano ni sawa na hamna kitu,kwa ujumla tuseme tayari yashapitishwa sema tu wanaidhinisha na kukaa kikao ili wapate per-diem zao,hii idea itakuwa imetolewa na wakenya kwa kushirikiana na rwanda na kwa sababu tz ni watu wa hewala hewala tushaingia kingi,kwa ujumla baada ya kuanza kutumia hiyo pesa moja tanzania tutapigwa bao sana na nchi hizi mbili kwani pesa yetu iko chini sana ukilinganisha na ya kwao.sijui lakini mi naona ni kama njia nyingine ya kuwabebesha mzigo wananchi tu,ukiangalia sweden mpaka leo wanasita kuingia kutumia euro moja kwa moja sababu ni hiyo hiyo ambayo tunatakiwa tanzania tuitumie,lakini wapi bwana kwa viongozi wetu walivyo vilaza.kwanza sipati picha watakavyokuwa wanasinzia kwenye hayo majadiliano badala ya kusikiliza na kuuliza kama si kuweka pingamizi panapohitajika,vibosile wetu watasinziaa weee wakati wenzao wakenya na rwanda na uganda wanafanya maamuzi,wakijashtuka kikao kishaisha na wakiulizwa maoni wanaishia kukubali kilakitu na kumwaga saini.basi tumeshaliwa,
nyie subirini mtanambia kama haijatokea hivyo.tutege masikio

No comments:

Post a Comment