Wednesday 12 January 2011

HUU MWAKA MNAUONAJE BANDUGU??




kwanza tutakiane heri ya mwaka mpya(kwenu hasa nyinyi mliopata heri),kwangu mimi naona mwaka umeingia ki-balaa balaa tu,mambo ni vangala vangala kama kitu gani sijui,kwanza jioni hiyo hiyo ya kuusubiria mwaka 2011 nikapata mgonjwa.baaasi mambo yote ya mipakazo na kupakaza yakaishia hapo nikawa mpole nikasema labda kesho yake tar 1 itakua ahueni.aaaah kuamkia tar 1 mgonjwa wangu ndo kwaaaanza hali ikazidi kuweka msisitizo kwamba safari hii hakuna kutoka daah.kwa ujumla ikabidi nyumba iwe nursing home kwa muda wote huo.nikajikalia home nikashukuru mungu hata hivyo(huku nikijichangamsha na viloba).anyway mwaka umeingia lakini kwangu sio njema kiivyo maana naona dalili tu za vijimambo vya hapa na pale sio nzuri,sijui itakuwaje huko mbeleni sijui ni swala la kukaza mkanda tu na kuendelea na maisha kama ilivyoimbwa na msondo"wanaume tumeumbwa mateso".sitaongea sana kuchelea kuchafua tena hali ya hewa kwa leo ntaishia hapo na kuanza kuukunjia ndita huu mwaka ili japo uogope kidogo kuniletea noma maana si unajua tena,ukiudekeza utajikuta umegalagazwa na kujikuta uko kwenye vijiji vya ujamaa na kujitegemea kama kule kwetu "kyimo kijiji kitulifu"unalima ndizi na maharage.sijui kwenu nyinyi mnauonaje wadau?tuambizane

8 comments:

  1. huu mwaka si mbaya wabaya watu.ila watajijeijei havutwi mtu mguu mwaka huu hata kidogo.formula ni ifuatavyo;kazi(focus)+maendeleo</#µ€()½§§§ family=mafanikio mwaka mzima.

    ReplyDelete
  2. safi sana mdau wangu hapo umenifurahisha kwa ushauri wako,hasa mahesabu yako pale mwisho.nafikiri ntatumia hiyo formula.thanx

    ReplyDelete
  3. Yaani wee kukaa na mkeo mkesha wa mwaka mpya unaona ilikuwa balaa?. Ulitamania uende viwanja upigwe ngumi au? Mshukuru Mungu kwa yote na endelea kuganga njaa utafanikiwa. Acha kulalamika na kulamumu bila sababu.

    ReplyDelete
  4. sijalaumu mdau umenielewa vibaya,nimesema nilikubaliana na hilo,ninachosema mwaka umeingia vibaya ni mambo yaliyonitokea tena baada ya hapo,siwezi kusema ila ndio yaliyofanya niseme mwaka unakuja vibaya.

    ReplyDelete
  5. hahahahaha watu bwana kama nilivyosemahapo mwanzo.WABAYA. haya ukisema wao wamaanisha lile tutaelewana vipi?....basi akaaaaa we unaweka formula ile moto na moto wake.

    ReplyDelete
  6. nimechoka,kwanza hata sijataja mgonjwa alikuwa yupi,lakini raia washanitajia dih.

    ReplyDelete
  7. asante mumy losh tumepona sasa tuko wazima kabisa maisha yanaendelea.

    ReplyDelete