Monday 19 December 2011

HEKA HEKA ZA MASTAA BONGO

USIKU wa kuamkia Jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita, ufukwe wa Hoteli ya Sun Rise, Kigamboni, Dar es Salaam, ulitawaliwa na hekaheka za mastaa wa muvi za Kibongo.
Ijumaa Wikienda liliwashuhudia mastaa hao wakijiachia kwenye sherehe ya kufunga mwaka 2011 ya kampuni ya Steps Entertainment inayojishughulisha na usambazaji wa kazi zao.
Katika ‘iventi’ hiyo, gazeti hili lilinasa baadhi ya matukio interesting;
Jenifer, Kanumba, Ray mmh!
Msanii mwenye umri mdogo, Hanifa Daud ‘Jenifer’ alifungua hekaheka hizo kwa kuwachokoza  magwiji, Steven Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray’.
“Anko Kanumba yule pale Anko Ray, umemuona? Hebu twende tukapige naye picha,” Jenifer alimwambia Kanumba ambaye alionekana kupotezeana na Ray kwani kila mmoja alikuwa kivyake tofauti na ilivyozoeleka (kama kuna bifu la chini ya kapeti).
Wolper amkwepa Wema na Zamaradi
Wakati shughuli hiyo ikiendelea, Jacqueline Wolper alionekana kukwepana na Wema Sepetu pamoja na mtangazaji wa Clouds TV, Zamaradi Mketema ambapo wakati wote alikuwa kimya hadi muda wa kuondoka ulipowadia akaondoa gari kwa kasi ya ajabu.

Richa Adhia aanika siri zake za kimapenzi
Miss Tanzania 2007, Richa Adhia aliweka wazi kuwa amekuwa akimsisitiza mwanaume wake (Peter wa Japan) kutumia kinga wanapokuwa kwenye ‘malavidavi’ ili kuepuka mimba isiyotarajiwa.”
Rose Ndauka amwanika wake kwa mastaa
Rose Donatus Ndauka, aliamua kumwanika mchumba wake, Malick Bandawe kwa baadhi ya mastaa huku wengine wakimsihi kuwa mtulivu zaidi kwani muda wa kuruka na wanaume tofauti umeshaisha.
WASTARA, SAJUKI HUREEE!
Hatimaye kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi kadhaa, Wastara Juma alionekana mwenye furaha akiwa na mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye alikuwa mgonjwa na afya yake kuzorota akisumbuliwa na maradhi ya uvimbe tumboni.

TOKA:IJUMAAWIKIENDA

No comments:

Post a Comment