Thursday 8 December 2011

TIMU YA TAIFA LEO IMEKUNYWA VIKOMBE 3-1 VYA UGANDA


Mi si mshabiki sana wa mpira na kilichosababisha ni hiki kwamba hatuna timu ya kushabikia,timu yetu imekuwa kibonde wa kupigwa mabao kama vile wameokotwa mtaani na kuingizwa uwanjani kucheza na timu kali.
nna swali moja najiuliza hivi bado kuna mzalendo kabakia kuwashangilia hawa jamaa?maana naona siku hizi hawakopeshwi wakishalambwa bao tu watanzania wazalendo wote wanageuza kibao na kuanza kushangilia timu pinzani huku wakiizomea timu yao ya taifa
yes haya ni maendeleo ya sayansi na tekenolojia maana siku hizi washabiki sijui wamelishwa nini.

tufanyeje ili timu yetu iweze kusonga mbele japo kiduchu?
mi naona bora tuendelee kuwazomea kila wanapofungwa mpaka siku waone aibu kuingia uwanjani kama hawana hakika ya ushindi

NI WAZO TU

No comments:

Post a Comment